Monday, 8 December 2014

AGUERO ASEMA ATAKAA NJE KWA MWEZI MZIMA


Mshambuliaji nyota wa Man City, Sergio Aguero amemuambia rafiki yake atakuwa nje kwa mwezi mzima kutokana na maumivu ya goti.


Aguero aliumia katika mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton.

Tayari Man City imeshatangaza kuwa ameondolewa kwenye kikosi kitakachopiga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AS Roma, Jumatano.


Hata hivyo, imeelezwa Aguero atafanyiwa vipimo ndani ya siku chache ambavyo vitaamua matibabu yake yafanyike kwa muda gani na akae nje kwa kipindi kipi.

0 comments: