Mwigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji amefunguka kuhusu hatma ya maisha yake ya ndoa na kuelezea ni kwa nini hana haraka ya kuingia katika maisha hayo kwa sasa.
Kwa mujibu mahojiano aliyofanyiwa na Gazeti la Vanguard la Nigeria amesema ndoa sio kitu cha kukurupuka na kinahitaji muda zaidi katika kujipanga na kutekeleza.
“Endapo nitaolewa,natamani sana nidumu kwenye ndoa yangu na kudumu kwake najua si kazi ndogo inahitaji uvumilivu mkubwa,nafahamu unapoingia unatakiwa kufahamu kile ni kifungo cha moja kwa moja na mwenzako ndio wa kufa na kuzikana hivyo tunapaswa kutambua kuna shida na raha zake na pia tunapaswa kujifunza kusamehe na kusahau endapo tunakwazana na wenza wetu,”alisema Genevieve.
0 comments:
Post a Comment