Saturday, 13 December 2014

LIVE KUTOKA TAIFA;...YANGA 0 VS SIMBA 2 (FULL TIME)

 

MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAA
Dk 89, Mrwanda anaangushwa, Niyonzima anapiga lakini Ivo anadaka kiulaiiinii

Dk 87, mashabiki Yanga wanaanza kutoka uwanjani, Simba wanawazomea
Dk 86, Simba wanamtoa Simon Sserrunkuma na kumuingiza Shabani Kisiga

Dk 84 Simba wanamtoa Maguri, nafasi yake inachukuliwa na Danny Sserunkuma. Mwamuzi anampa Maguri kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 78 Yanga inamtoa Juma Abdul na kumuingiza Javu

Dk 76, Ngassa anapiga krosi lakini inaishia mikononi mwa Ivo Mapunda

Dk 72, Simba wanamtoa Messi na nafasi yake inachukuliwa na Said Ndemla
Dk 65, Simba wanamtoa Tshabalala Mohammed Hussein aliyeumia, nafasi yake inachukuliwa na Issa Rashid 'Baba Ubaya'
Dk 66, Mrwanda anapiga mpira langoni kukiwa na mabeki tu, Owino anaruka juu na kuokoa kwa kichwa.

Dk 65 Yanga wanamuingiza Mrisho Ngassa kuchukua nafasi ya Mliberia Sherman aliyeumia

Dk 63, Mliberia Sherman anatoka nje mwenyewe baada ya kuumia. Awali alirudi, lakini anaonekana kuzidiwa
Dk 56, Yanga inamuingiza Salum Telela na kumtoa Mbrazil, Emerson

Dk 52 Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mbele ya Messi Singano. Simba bado wanatawala katikati ya uwanja

Dk 49, Sherman anawaacha mabeki wa Simba, wanamuangusha, inakuwa faulo inayookolewa na mabeki wa Simba
Dk 48, Msuva anapiga shuti kali lakini mpira unazuiwa
Dk 46 Simba wanamtoa Murishi wanamwingiza Joseph Owino
          Yanga wanamtoa Coutinho wanamwingiza Danny Mrwanda
MAPUMZIKO
GOOOOOOOO Dk 41 Maguri anaifungia Simba bao baada ya kuunganisha mpira wa kurusha wa chollo ambao uligonga mwamba, mabeki wa Yanga wakazubaa, akarudi na kufunga tena.


Dk 40, Yanga wanamtoa Twite aliyeumia, nafasi yake anachukua Hassan Dilunga

Dk 33, Coutinho anapiga shuti saafi lakini linatoka nje sentimeta chache

GOOOOOOOOOOOOO DK 30, Awadhi Juma anauwahi mpira wa faulo wa Okwi na kuukwamisha wavuni ilikuwa ni baada ya Dida kuutema.

Dk 25 Sherman anampa pasi nzuri Msuva naye anaachia shuti kali lakini linapiga nyavu za nje.

Dk 23, Sherman anagongeana vizuri na Msuva na kutoa pasi nzuri....lakini hakuna mmaliziaji
Dk 17, Okwi anawachambuamabeni wawili wa Yanga lakini anaangushwa na kuwa faulo, anaipiga Okwi...goal kick

Dk 13 vurugu zinazuka, lakini mwamuzi anachukua maamuzi magumu na kutotoa kadi...ubabe unatawala
Dk 11 Emerson anapiga krosi safi lakini Coutinho anaukosa mpira
Dk 7, Sherman anawachambua mabeki watatu wa Simba lakini anashindwa kumalizia


Dk 5, Sserunkuma Jr anatolewa nje anatibiwa baada ya kugongwa na Yondani
Dk 3, Yanga wanafanya shambulizi, Sherman anampa pasi nzuri Msuva anapiga shuti linadkwa na Ivo

Dk 2, Okwi anapiga mkwaju wa faulo lakini unadakwa vizuri na Dida.

VIKOSI VYA LEO YANGA VS SIMBA
YANGA:
Deo Dida
Abdul Juma
Oscar Joshua
Nadir Haroub
Kelvin Yondani
Mbuyu Twite
Haruna Niyonzima
Emerson Roque
Simon Msuva
Kpah Sherman
Coutinho

SIMBA:
Ivo Mapunda
Nassor Chollo
Mohammed Hussein
Hassan Isihaka
Juuko Murishid
Jonas Mkude
Rama Singano
Awadh Juma
Elius Maguri
Simon Sserunkuma
Emmanuel Okwi

0 comments: