jaji Francis Mutungi
Na Amina Azizi wa radio uhuru Fm, Dar es Salaam
Msajili
wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji FRANCIS MUTUNGI, amekemea vurugu na
vitendo vya uvunjifu wa amani vilivyotokea maeneo ya Mahakama Kuu, Kanda
ya Dar es salaam, baada ya kusikilizwa na kutolewa uamuzi wa kesi ya
ZITO KABWE.
Kauli
hiyo imekuja kufuatia hivi karibuni wafuasi wanaomuunga mkono ZITTO na
wengine uongozi wa CHADEMA kufanya vurugu katika maeneo ya Mahakama Kuu
jijini Dar es Salaam.
Jaji
MUTUNGI amekemea suala hilo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari
aliyoitoa leo, kuhusu vitendo vya vurugu vilivyotokea katika maeneo ya
Mahakama hiyo baada ya kusikiliwa na kutolewa uamuzi wa kesi ya ZITTO
dhidi ya CHADEMA.
Kupitia
taarifa hiyo Jaji MUTUNGI amewaasa viongozi wa CHADEMA na ZITTO kuzuia
wafuasi wao kujihusisha na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani wa
aina yoyote wakati wote ambapo mgogoro baina yao ukiwa bado unaendelea.
Amesema
migogoro ndani ya vyama vya siasa ni moja wapo ya vyanzo vya uvunjifu
wa amani hivyo amewaasa wadau wote kwamba migogoro hiyo inapaswa isivuke
mipaka na kuwa uhasama na uadui wa kufanya wafuasi wa pande mbili
kupigana kwani hiyo sio demokrasia.
Hata hivyo
amewataka viongozi wa vyama vya siasa kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa
kushughulikia tofauti zao na migogoro baina yao kwa ustaarabu, utulivu
na amani huku wakizingatia sheria zote za nchi.
Sheria
ya Vyama vya Sisa namba 5 ya mwaka 1992 na kanuni za maadili ya vyama
vya siasa za mwaka 2007 inakataza vyama vya siasa kuruhusu wanachama au
mashabiki wake kujihusisha na vitendo vya vurugu na uvunjifu wa amani wa
aina yoyote ile.
0 comments:
Post a Comment