Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
JESHI
la Polisi Mkoani Singida linamshikilia mfanyabiashara mmoja kwa tuhuma
za kupatikana na noti bandia za shilingi 10,000 na 5,000 zenye thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 3.4 milioni
Mtuhumiwa
huyo Toye Wagela (39) mkazi wa kijiji cha Mitale mkoa wa Kigoma
amekamatwa juzi saa nane mchana wakati akijaribu kununua chakula kwenye
hotel moja wilayani Manyoni Mkoa wa Singida.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Singida,SACP Geofrey Kamwela amesema kuwa baada ya
mtuhumiwa kutoa moja ya noti hizo na kutiliwa shaka alianza kujaribu
kukimbia kabla ya kukamatwa na wananchi.
Amesema
kuwa wananchi hao waliita polisi ambapo baada ya kupekuliwa kwenye
mifuko ya suruali, mtuhumiwa alikutwa na noti 200 za shilingi 10,000 na
nyingine 209 za shilingi 5,000.
Kamanda
Kamwela amesema wanaendelea kufanya uchunguzi wa kina na kuwatafuta
washirika wengine wa uhalifu huo,kabla ya mtuhumiwa kupandishwa
kizimbani kujibu tuhuma ya kupatikana na noti bandia.
0 comments:
Post a Comment