Monday, 20 January 2014

MOHAMED MORSI AFUNGULIWA MASHTAKA ZAIDI

Mohamed Morsi 
 Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi wa kundi la Muslim Brotherhood mjini Cairo, Jan. 8, 2014.
Wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi wa kundi la Muslim Brotherhood mjini Cairo, Jan. 8, 2014.
Rais wa Misri aliyeondolewa madarakani Mohamed Morsi  tayari anashtakiwa kwa shutuma za kuchochea ghasia pia atashtakiwa kwa makosa ya kuidhalilisha mahakama.


Rais huyo wa zamani tayari amefunguliwa mashtaka kwa kuchochea ghasia ambazo zimesababisha vifo vya waandamanaji. Pia anakabiliwa na kesi nyingine mbili, moja kwa shutuma za upelelezi  na nyingine kwa kuandaa mpango wa kuvunja  gereza moja. Viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood la bwana Morsi pia wanakabiliwa na mashtaka kama hayo.


Jeshi la Misri lilimuondoa madarakani bwana Morsi mwezi Julai wakati upinzani ulipomshutumu kwa kujilimbikizia madaraka mengi. Wamisri walipiga kura kwa kauli moja kuunga mkono  kura ya maoni wiki iliyopita ili kupitisha  katiba  mpya ambayo itachukua nafasi ya ile ambayo inaungwa mkono na wafuasi wa bwana morsi. Uchaguzi wa rais mpya na wabunge unatarajiwa kufanyika baadae mwaka huu.

Related Posts:

0 comments: