Monday, 20 January 2014

MABADILIKO MAWAZIRI:TUNASUBIRI MAENDELEO YA HARAKA SIO SIASA

kikwete 55590
Jana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri ikiwa ni baada ya mawaziri watatu kutenguliwa nafasi zao na mmoja kujiuzuru kutokana na oparesheni tokomeza ujangili na mwingine kufariki.
Mawaziri hao aliyekuwa wa Maliasili na utalii, Balozi Hamis Kagasheki, wa Fedha Dkt. William Mgimwa, wa Ulinzi Shamsi Vuai Nahodha, wa Mifugo David Mathayo na wa Mambo ya ndani Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Mabadiliko hayo yaliyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue yamewaacha watano, wanne kuwapandisha kuwa mawaziri kamili na kuwaongeza wapya 10 wakiwemo mawaziri wawili na manaibu nane na mawaziri waliohamishwa ni nane. (HM)

Wengine kukwama kutokana na sababun zilizo nje ya uwezo wao kama tatizo la fedha huwezi kumlaumu Waziri wa Fedha labda hakuna mapato ya kutosha kwa wakati huo.

Mawaziri hao ni Christopher Chiza (Kilimo, Mifugo na Ushirika), wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa, Naibu wake Adam Malima, wan chi ofisi ya Waziri mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia na Manaibu wake Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa. Kati ya hao aliyehamishwa ni Malima ambaye amekuwa Naibu wizara ya fedha huku wengine wakibaki katika nafasi zao.

Kitendo hicho kinaonesha kuwa si jambo jema kuwazungumzia viongozi hadharani kama walivyofanya viongozi wa CCM hali ambayo wangeweza kuimaliza kupitia vikao vya ndani kama Katibu mkuu mstaafu, Yusuph Makamba alivyoshauri.

Lakini pia kwenye ukweli uongo hujitenga, tusubiri tuone nani mkweli kati ya pande mbili hizi ule wa wananchi, wabunge na viongozi wa CCM waliokuwa wakidai Mawaziri mizigo na ule wa Rais na mamlaka yake.

Mabadiliko yamefanyika, tusubiri kuona utendaji kazi wao katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kinachotakiwa ni kutofanya kazi kwa mazoea. Wahenga wanasema ni samaki aliyekufa tu ndio anaogelea kufuata maji yanakokwenda.

Wananchi wanahitaji maendeleo ya haraka na uhakika si kupiga maneo yasiyoendana na vitendo.
Tuwape nafasi waweze kuonesha uwezo wao wa kiutendaji kwa kufuata misingi ya haki na utawala wa sheria. \

Chanzo: Hakimu Mwafongo

Related Posts:

0 comments: