Sura mpya 10 ndani
Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi
Rais Jakaya Kikwete, jana alifanya mabadiliko ya
katika Baraza la Mawaziri kwa kujaza nafasi tano zilizokuwa wazi huku
akiziteua sura mpya 10, watano kuwatema na wizara sita zikibaki kama
zilivyo.
Aidha, katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amewahamisha mawaziri wanane kwenda wizara nyingine.
Akitangaza mabadiliko hayo Ikulu jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais Kikwete, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema Rais amejaza nafasi za wizara zilizoachwa wazi baada ya mawaziri wake kujiuzulu na wengine kutakiwa kujiuzulu.

HAWA NDIO WALIOPIGWA CHINI
Waliong’olewa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Godlucky Ole Medeye, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Benedict Ole Nangoro na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gregory Theu.
SURA MPYA
Katika uteuzi huo, sura mpya ni Dk. Kamani, Ole Telele na Mgimwa, na Dk. Asha-Rose Migiro, ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Kabla ya uteuzi huo, Dk. Migiro alikuwa Mbunge wa kuteuliwa na aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN). Aliwahi pia kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Aidha, aliwahi kuwa Mbunge Viti Maalumu.
Vile vile hivi sasa Dk. Migiro anashikilia nafasi ya ukatibu wa Siasa na Mambo ya Nje katika Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Rais Kikwete pia amemteua Mwigulu Nchemba kuwa Naibu Waziri wa Fedha. Nchemba ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara.
Wengine ni Jenista Mhagama ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Mhagama pia ni Mbunge wa Peramiho (CCM) na Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania.
Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Pindi Chana, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, akichukua nafasi ya Ummy Mwalimu, aliyehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Rais kuwa Naibu Waziri (Muungano).
Chana ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa, pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Katiba, Sheria na Utawala.
Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, anakuwa Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika akichukua nafasi ya Adamu Malima, aliyeahamishiwa Wizara ya Fedha.
Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia anakuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Nkamia kabla ya kuwa mbunge aliwahi kuwa Mwanahabari wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), lakini pia amefanya kazi Voice of America Marekani.
Dk. Kebwe Stephen Kebwe anakuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Seif Rashid ambaye amepandishwa na kuwa Waziri wa wizara hiyo.
Katika mabadiliko hayo, Wizara ambazo hazikuguswa ni Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Uchukuzi, inayoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe na Naibu wake ni Charles Tizeba; Ujenzi, Dk. John Magufuli amebaki na Naibu wake, Gerison Lwenge.
Nyingine ni Wizara ya Kazi na Ajira, ambayo waziri wake ni Gaudencia Kabaka na Naibu wake ni Dk. Makongoro Mahanga.
Pia ni Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambayo itaendelea kuongozwa na Prof. Makame Mbarawa na Naibu wake, Januari Makamba huku Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikiendelea kuongozwa na Samuel Sitta na Naibu wake Abdullah Juma. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatiafa itaendelea kuwa chini ya Bernard Membe na Naibu wake, Mahadhi Juma Maalim.
Zilizofanyiwa mabadiliko ya manaibu Waziri ni Charles Kitwanga, anayekuwa Naibu Waziri wa Nishati akitokea Ofisi ya Makamu wa Rais; Amos Makalla anayekuwa Naibu Waziri wa Maji akitokea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wengine ni George Simbachawene, ambaye amehamishiwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa Naibu Waziri na akitokea Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha, Katika uteuzi huo, aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, amepandishwa na kuwa waziri kamili.
AMBAO HAWAKUGUSWA
Mawaziri ambao hawajaguswa na mabadiliko hayo ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe; Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Naibu wake Stephen Masele na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa.
Wengine ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda; Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba; Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Wengine ni mawaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Stephen Wasira (Mahusiano na Uratibu); George Mkuchika (Utawala Bora); Prof. Mark Mwandosya (Kazi Maalumu) na Celina Kombani (Menejimenti ya Utumishi wa Umma).
Upande wa ofisi ya Waziri Mkuu mawaziri wote wamebaki. Mawaziri hao ni Dk. Mary Nagu (Uwekezaji na Uwezeshaji); William Lukuvi (Sera, Uratibu na Bunge); Hawa Ghasia (Tamisemi) na Naibu wake, Aggrey Mwanri pamoja na Kassim Majaliwa (ELimu)
AWATETEA MAWAZIRI MIZIGO
Balozi Sefue alisema suala la mawaziri mizigo, Rais analipima katika utendaji wa mtu binafsi na yale matatizo yanayosababishwa na wasaidizi wa waziri au naibu wake.
Alisema wapo mawaziri ambao binafsi hawana tatizo lolote, lakini wanaangushwa na watendaji wa chini yao na kwamba si rahisi kuwaondoa kwa kuwa ni wachapakazi lakini wanakosa msaada kutoka kwa wasaidizi wao.
“Yapo mambo ambayo yapo nje ya uwezo wa Mawaziri husika, ni ngumu kuwalaumu na kuwaita mzigo wakati ni suala gumu kwao, mfano uhaba wa fedha si suala la kuliita tatizo la waziri, hivyo inategemea…kila wizara ina matatizo tofauti,” alisisitiza Sefue alipoulizwa kuhusiana na baadhi ya mawaziri waliolalamikiwa kutoondolewa katika nafasi zao.
Alisema rais amefanya mabadiliko hayo ili kuimarisha utendaji na kupanga timu yake vizuri katika kuwatumikia Watanzania na siyo vinginevyo.
Baadhi ya mawaziri walioalamikiwa na wananchi kwa viongozi wa sekretarieti ya CCM kutokana na utendaji mbovu ni Chiza, Malima na Dk. Kawambwa.

SOURCE:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment