Moto
mkubwa uliosababishwa na hitirafu ya umeme umewaka eneo la
Mwananyamala Jirani na Hospitali ya Mwananyamala na kusababisha kuungua
kwa Maduka matatu pamoja na nyumba moja ambayo ilikuwa imeungana na duka
moja wapo ambamo walikuwa wanauza vitambaa na kushona nguo.
Moto
huo ulichukua zaidi ya masaa mawili ambapo wakazi wa eneo hilo ndio
waliosaidia kwa kiasi kikubwa kuzima moto huo mpaka kuumaliza na baadae
Kikosi cha kuzima moto kufika na kukuta moto ndio unaishia na kuendelea
kumalizia kushirikiana na wananchi wengine kuzima moto huo.
Katika
tukio la Moto huo hakuna mtu ambaye amedhuriwa ingawa katima maduka
yote matatu walifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu huku vilivyobakia
kuteketea vibaya kwa moto huo.
Moto ukiwa umeanza kama utani, watu wakiwa wanaendelea na kazi kama kawaida.
Moshi ukiwa unazidi katika eneo ambalo maduka matatu yameteketea kwa moto.
Gari likiwa linarudi nyuma lilipotokea baada ya kuona kuna moshi mkubwa mbele yao.
Mashuhuda wakiwa wameanza kuelekea eneo la tukio
Moto ukiwa unaanza kupamba moto, waya wa umeme unao onekana unashuka chini ndio umesababisha moto huo.
Moto ukiwa unazidi pamba moto katika duka la kushonea nguo na kuuza vitambaa.
Duka
la nguo likiwa linapamba moto na maduka mengine yakiwa yameanza kupamba
moto pamoja na nyumba ambayo ilikuwa imeungana na duka.
Mmoja ya vijana akiwa anaanza kuokoa vitu vyake jirani na maduka yaliyokuwa yakiungua.
Moto ukiwa unazidi
Baadhi ya Mashuhuda wakimwagiwa maji kupisha njia ya waokoaji waliojitolea kuzima moto kupita
Mmoja wa Mashuhuda akiwa anachukua tukio kwa umakini
Kikosi
cha zima moto wakiwa wakiwa wanawasili eneo la tukio, huku wananchi
wakiwazuia wasifanye kazi kwa kuwa kazi wamekuta imeisha
Kikosi cha zima moto wakiwa wameanza shuguli ya kumalizia kuzima moto
0 comments:
Post a Comment