Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko
nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao
ni na Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye
televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa
Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa
pili kushoto) na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na
msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya
Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko
nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao
ni na Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye
televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa
Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa
pili kushoto) na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na
msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya
Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii
nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya
kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni Terrence J.
(Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E!
Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton,
Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group.
Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya
Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki,
mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo
maarufu ya Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha ya pamoja na wasanii hao.
……………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu Julai 14, 2014
amekutana na kundi la wasanii kutoka Marekani lililowasili nchini usiku
wa Alhamisi, Julai 10, 2014, kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa wasanii
wa Tanzania kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mjini Dar es
Salaam.
Wasanii hao ni pamoja na Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa
kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa
filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za
Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group.
Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka
Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji,
mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata
kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Kiasi cha wasanii 250 walishiriki semina hiyo inayoitwa Mafunzo
ya Uendelezaji Usanii. Hiyo ilikuwa ni kutimiza ahadi aliyotoa Rais
Kikwete kwa wasanii wa Tanzania kuwa atachangia kuinua kiwango cha ujuzi
na weledi wao kwa kuwaandalia mafunzo yatayoendeshwa na magwiji wa
sanaa kutoka Marekani sasa imetimia.
Akizindua Kampeni ya Uzalendo kwa Vijana inayoendeshwa na
Muungano wa Wasanii Tanzania kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwezi
uliopita, Juni 14, 2014, Rais Kikwete aliahidi kuchangia kuinua kiwango
cha usanii na weledi wa wasanii wa Tanzania kwa kusaidia kuandaa
mafunzo yatakayoendeshwa na wasanii maarufu kutoka Marekani.
Mbali na kuendesha shughuli za mafunzo ya wasanii ambazo
wamekuwa wakizifanya kwa makundi madogo madogo tokea walipowasili
nchini, pia wanamuziki hao wa Marekani na kundi la wapiga picha
watatembelea sehemu mbali mbali nchini, hasa kwenye vivutio vya watalii,
ambako watapiga picha na kuandaa vipindi vya kuitangaza Tanzania katika
vyombo vya habari vya Marekani.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
15 Julai,2014
0 comments:
Post a Comment