Monday, 20 January 2014

VITUKO KIAPO KWA MAWAZIRI WATEULE WA JK MMOJA ACHEMKA KUAPA IKULU DAR LEO

 

HAFLA FUPI YA KUWAAPISHA MAWAZIRI WAPYA IKULU DAR LEO

Rais Jakaya Kikwete na Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal wakiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri Mbalimbali wapya mara baada ya kuwaapisha kwenye viwanja vya ikulu leo ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na waalikwa wamehudhuria na kushuhudia Picha na OMR 02 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimpongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akiwa na mkewe aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Faraja Kotta na  familia yake, baada ya kuapishwa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kulia kwa Makamu ni Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.  Picha na OMR 003 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Adam Malima, kuwa Naibu Waziri wa Fedha, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 03 
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Charles Kitwanga, kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 005 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Amos Makala, kuwa Naibu Waziri wa Maji, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jenista  Mhagama, kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 007 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Dkt. Pindi Chana, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 008 
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mwigulu Nchemba, kuwa Naibu Waziri wa Fedha, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha    009 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Juma Nkamia, kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 10 
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mahmoud Mgimwa, kuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 11 
Baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali wakiwa katika hafla hiyo. 12 
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo

VIOJA mbali mbali  vimejitokeza wakati wa mawaziri  wateule wa Rais Dr Jakaya  Kikwete  wakila  kiapo baada ya  naibu  waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi mbunge wa Peramiho mkoani Ruvuma Jenista Mhagama  kulazimika  kula  kiapo  kurudia  kiapo mara tatu tofauti na  wenzake ambao  waliapa mara mbili kutokana na  naibu waziri  huyo kuchemka mara ya  kwanza mbele ya Kikwete .

Mbali ya Mhagama  kuchemka na kuingia katika  rekodi ya kurudia kiapo mara tatu pia naibu katubu mkuu wa CCM ambae ni naibu waziri wa fedha Bw Nchemba yeye  alitinga katika viwanja  hivyo  huku akiwa kawaida na  jezi  za timu ya Taifa tofauti na wengine ambao  walifika  wakiwa  wameulamba  suti vikali .

Hata   hivyo  wapembuzi wa mambo  wanadai  kuwa  kuchemka kwa Mhagama  katika zoezi hilo ni kutokana na kutokuwa na imani kama angeteuliwa  kuingia kushika nafasi hiyo  nyeti na  unaibu  uwaziri 

Related Posts:

0 comments: