>>YAFANYA WALICHOWAFANYIA SPURS KWA WILLIAN!
>>CHELSEA YAKUBALIANA NA BASEL KUMSAINI MOHAMED SALAH WA MISRI!
>>SASA DILI YA MATA KUTANGAZWA RASMI!
Salah, Miaka 21, bado hajapimwa Afya
wala kukubaliana Maslahi yake binafsi na Chelsea lakini anatarajiwa
kuhamia Stamford Bridge.
Ilikuwa sio siri kuwa Liverpool ndio
walioanza mazungumzo na Basel, Mabingwa wa Uswisi, ili kumchukua Salah
lakini sasa Chelsea wamefanya kile kilichowakuta Tottenham
‘waliponyang’anywa’ Kiungo Willian kutoka Anzhi ya Urusi Dakika za
mwisho.
Jana Chelsea ilifikia Makubaliano na
Manchester United kuwauzia Juan Mata na Dili hii ilicheleweshwa
kuthibitishwa na Klabu hizo mbili ikiaminika Chelsea wanangoja
kukamilisha Uhamisho wa Salah ili Uhamisho wa Mata utangazwe rasmi!
Salah anakuwa Mchezaji wa Pili Chelsea
kumsaini kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari na mwingine ni Nemanja
Matic aliesaini kwa Pauni Milioni 21 kutoka Benfica Wiki iliyopita.
Salah, ambae aliifunga Bao Chelsea
walipocheza na Basel kwenye Nusu Fainali ya Europa Ligi Msimu uliopita
na pia kuiipiga Bao kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu huu, anang’ara mno
huko Uswisi na amekuwa akiwindwa na Klabu kubwa Barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment