>>NI KUFUATIA KUTINGA MAHAKAMANI WAKICHUNGUZWA UBADHIRIFU UHAMISHO WA NEYMAR!
Inadaiwa Rosell alilipua uamuzi huo
wakati alipotembelewa na Josep Maria Bartomeu na Javier Faus, ambao wote
wawili ni Makamu wa Rais wa Barca.
Hata hivyo, Usiku huu kipo Kikao cha
Dharura cha Bodi ya Klabu ambacho kitajadili nini mustakabali wa Klabu
kufuatia kutinga Mahakamani wakichunguzwa kwa Ubadhirifu wa Fedha kwenye
Uhamisho wa Supastaa wa Brazil Neymar kutoka Santos kwenda Barca
mwanzoni mwa Msimu.
Tuhuma dhidi ya Barca na Rosell ni
gharama halisi za Uhamisho wa Neymar ambao Barca walitangaza kuwa ni
Uhamisho wa Dau la Euro Milioni 57.1 wakati yapo madai ni zaidi ya hapo
na yapo malipo ya siri yaliyofanyika.
Kesi hii, itasikilizwa na Jaji Pablo Ruz
ambae anatarajiwa kukusanya taarifa toka kwa Neymar, Santos na
Barcelona kabla hajamwita Rosell aende mwenyewe Mahakamani kutoa
Ushahidi.
Kesi hii inafuatia malamiko ya
Mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases, ambae ameungwa mkono na Waendesha
Mashitaka wa Spain waliokubaliana na Madai yake kwamba kulikuwepo
ubadhirifu na ukiukwaji wa Sheria kwa kutumia Mkataba Feki.
Pia, wametaja Kitita cha Euro Milioni 40
kilicholipwa kwa Kampuni ya Baba yake Neymar ambacho hakikutangazwa
katika Uhamisho huo.
Juzi Jumatatu, Gazeti maarufu huko Spain, El Mundo, lilitoboa
kuwa Dau halisi la kumnunua Neymar ni Euro Milioni 95 kitu ambacho
kilimfanya Rais Sandro Rosell atake nafasi Mahakamani ili atoe ushahidi
na kujisafisha.
Hiyo Jumatatu, Rosell, akiongea na
Wanahabari alitamka: “Kuna vitu viwili nataka kusema. Kwanza Neymar
aligharimu Euro Milioni 57.1. Na hili nimesema mara nyingi. La pili, ni
ombi, kwa heshima namuomba Jaji aniite ili nitoe ushahidi na kumwambia
kila kitu anachotaka kujua kwa sababu hamna cha kuficha!”
Katika kuisikiliza Kesi hii, Jaji Pablo
Ruz anatarajiwa kukusanya taarifa toka kwa Neymar, Santos na Barcelona
kabla hajamwita Rosell aende mwenyewe Mahakamani kutoa Ushahidi.
Rosell alishinda Uchaguzi wa Rais wa
Barca Mwaka 2010 na alitakiwa ashike wadhifa huo hadi 2016 lakini sasa
Nafasi hiyo itakamatwa na Bartomeu hadi Uchaguzi ujao.
0 comments:
Post a Comment