Thursday, 23 January 2014

MTOTO ALIYE PIGWA KWA KUA SURA YAKE HAFANANI NA BABA YAKE AMAFARIKI DUNIA

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja mkaazi wa Junguni Gando aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Wete akipatiwa matibabu baada ya kupigwa na baba yake kutokana na utofauti wa sura zao, amefariki dunia siku ya Jumatano saa10.30 alfajiri.

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Daktari wa Wodi ya Watoto wa hospitali hiyo, Sada Juma Mbwana zinasema, mtoto huyo amefariki dunia kutokana na majeraha aliyoyapata: “Mtoto alipofikishwa hospitalini tuliambiwa kwamba anasumbuliwa na kifua (anakohoa) lakini mambo yalikuwa mengine baada ya Polisi kufika wakiwa na PF3 na ndipo mama mzazi alipoeleza mwanawe amepigwa na baba yake,” alifahamisha Sada.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Shakhan Mohammed Shakhan amesema baba wa mtoto huyo anashikiliwa kutokana na tuhuma za kujeruhi, anatarajia kufikishwa mahakamini Jumatatu ijayo. --- MWANANCHI

 

0 comments: