ROBO FAINALI
Jumamosi Januari 25
[Saa za Bongo]
[Cape Town Stadium]
1800 Morocco v Nigeria
2130 Mali v Zimbabwe
Hii leo, Mechi zote zitachezwa Uwanja wa
Cape Town Stadium Jijini Cape Town kwa Morocco kucheza na Nigeria na
kufuatia Mali na Zimbabwe.
Morocco ndio walimaliza Kundi B wakiwa
kileleni kwa kushinda Mechi 1 na Sare 2 wakati Nigeria walimaliza Kundi A
wakiwa Nafasi ya Pili, nyuma ya Vinara Mali, kwa kushinda Mechi 2 na
kufungwa Mechi moja, kwenye Mechi yao ya kwanza, walipopigwa 2-1 na
Mali.
Nao Mali, waliomaliza Vinara Kundi A,
walishinda Mechi mbili na Sare 1 huku wapinzani wao Zimbabwe walitoka
Kundi B wakiwa Nafasi ya Pili kwa kushinda Mechi 1 na Sare 2.
Kesho Jumapili pia zipo Mechi mbili za Robo Fainali.
ROBO FAINALI
[SAA za Bongo]
Jumapili Januari 26
1800 Gabon v Libya [Peter Mokaba Stadium]
2130 Ghana v Congo DR [Free State Stadium]
NUSU FAINALI
Jumatano Januari 29
1800 Mali/Zimbabwe v Gabon/Libya [Free State Stadium]
2130 Ghana/Congo DR v Morocco/Nigeria [Free State Stadium]
Jumamosi Februari 1
1800 Mshindi wa Tatu [Cape Town Stadium]
2100 Fainali [Cape Town Stadium]
0 comments:
Post a Comment