Saturday, 2 August 2014

Bolt aisaidia Jamaica kufuzu


   
Usain Bolt
Bingwa wa mbio za mita 100 duniani Usain Bolt amelisadia taifa lake la Jamaica kufuzu katika fainali za 400 m x 100m hii leo licha ya tishio na kusisitiza kuwa amefurahi kuwa Glasgow.
Bolt amelazimika kukana madai kwamba alitoa matamshi mabaya dhidi ya mashindano hayo,ambapo nusra jamaica ishindwe baada ya mmoja ya wakimbiaji wake katika mbio za 400m X100m kupata jeraha.
Hatahivyo Bolt aliweza kuwasaidia wenzake na kushinda mbio hizo.
Bolt baadaye alikiri kwamba alifikiri kuna tatizo mahala .
Anasema kuwa alikuwa na wasiwasi lakini mwanariadha kimmari wa jamaica aliyeanza mbio hizo na kupata jeraha alimpokeza mwenzake kijiti cha kukimbia.
''Kocha wangu kwa mara nyingi hutuambia tukimbie na uchungu'',alisema Bolt.

0 comments: