Picha na Hussein
Makame-MAELEZO.
Meneja
Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa kampuni ya Bizfora
Investment Co. Ltd, John Matiko, akiwaeleza jambo wanahabari (hawapo
pichani) kuhusu Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo
yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa
Mlimani City jijini hapa. Kulia ni Mratibu wa Mkutano na Maonesho ya
Kimataifa ya Kilimo kutoka Kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd,
Dk.Ellen Otara-Okoedian. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Baadhi
ya wanahabari wakimsikiliza Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano wa kampuni ya Bizfora Investment Co. Ltd, John Matiko
(kushoto) kuhusu Mkutano na Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo
yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye ukumbi wa
Mlimani City jijini hapa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
Mmoja
wa wanahabari ambaye ni mpiga picha wa Televisheni ya Tumaini
(katikati), akiuliza swali kwenye mkutano wa wanahabari na kampuni ya
Bizfora Investment Co. Ltd iliyoandaa Mkutano na Maonesho ya Kimataifa
ya Kilimo yatakayofanyika kuanzia tarehe 10 April mwaka huu kwenye
ukumbi wa Mlimani City jijini hapa. Picha na Hussein Makame-MAELEZO.
………………………………………………………………………………………
Na Frank Mvungi-MAELEZO
TANZANIA
inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano na Maonesho ya Kilimo (AGRITECH)
2014, yatakayofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es
salaam kuanzia April 10 mwaka huu na kuwashiriksha waoneshaji wan je na
ndani ya nchi katika Nyanja mbalimbali za kilimo.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa mkutano huo Dkt.Ellen Otaru- Okoedian katika
mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa
Iadara ya Habari-MAELEZO leo jijini Dara es salaam.
Dkt
Ellen amesema mkutano huo unalenga uwezeshaji katika kilimo ambapo
wakulima wa Tanzania watapata fursa ya kukutana na wadau wakubwa wa
kilimo kutoka ndani na nje ya nchi ili kujadili na kuona namna bora ya
kuinua sekta ya kilimo nchini.
Alisema
mkutano huo pia utawahusisha wadau wa kilimo wakiwemo wauzaji wa
pembejeo,mbolea, na madawa ya mimea, matrekta, wanaohusika na
umwagiliaji, vyuo vya kilimo, biashara, za mazao, watafiti, Taasisi za
biashara za ndani na nje ya nchi, wakulima na wafugaji, Wizara zote
husika na mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali.
Aliongeza
kuwa katika mkutano huo unaotarajiwa kuanza tarehe 10 hadi 12 aprili
2014 wakulima watapata fursa ya kuelewa umuhimu wa zana bora za
kilimo,utafiti , jinsi teknolojia ya simu za mkononi inavyoweza kubadili
kilimo hapa nchini.
“Mkutano
huu pia utajadili fursa mbalimbali zilizopo kwenye kilimo na mchango wa
Taasisi za fedha katika kukuza kilimo hapa nchini na washiriki watapata
fursa ya kujadili na kutoa mawazo yao juu ya namna bora ya kuongeza
tija katika kilimo ili kupambana na janga la njaa hapa Tanzania na
Afrika kwa ujumla” alisema Dk. Ellen.
Dkt.
Ellen amesema mkutano huo utajumuisha washiriki toka mataifa takribani
20 yakiwemo Ujerumani, Marekani, Ufaransa, China, Japani, Kenya, Uganda
na Malawi.
Naye
Meneja Maonesho na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Kampuni
hiyo, John Matiko alitoa wito kwa wakulima hapa nchini na wadau wote wa
Sekta ya kilimo kujitokeza katika mkutano huo na pia kushiriki katika
maonesho yatakayofanyika wakati wa mkutano huo.
Kwa mujibu wa Matiko, mkutano huo utakuwa na Kaulimbiu isemayo “Nguvu ya Teknolojia katika Mapinduzi ya Kilimo”.
0 comments:
Post a Comment