Na Francis Godwin Blog
WASHIRIKI
wa warsha ya siku moja ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa
sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA) mkoani Iringa wamepongeza jitihada
mbali mbali zinazoendelea kufanywa na SSRA katika kuwakutanisha
wadau wa mifuko hiyo kwa kuwapa elimu zaidi.
Pongezi
hizo zimetolewa leo katika ukumbi wa VETA mjini Iringa na washiriki
wa warsha hiyo ambapo wameshauri mifuko mingine ya hifadhi ya
jamii kuiga mfano huo wa SSRA katika kuwapatia elimu wanachama wake
ili kutojutia kujiunga na mifuko hiyo.
Katibu
wa chama cha wafanyakazi wa sekta ya Kilimo Bw Deus Magesa
alisema kuwa jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na SSRA kwa
kuwatembelea wadau wake na kuwapatia elimu mbali mbali juu ya
mifuko hiyo pamoja na kupokea changamoto mbali mbali ila kwa mifuko
husika ambayo wanachama wamekuwa wakikatwa fedha zao imekuwa haina
utaratibu wa kutoa semina kwa wanachama wake.
Hivyo
alisema kuwa kama msimamizi mkuu wa mifuko hiyo SSRA amekuwa
akifika kutoa elimu iweje mifuko hiyo ya kijamii kama NSSF imekuwa
ikishindwa kufika kutoa elimu kwa wanachama wake na kuwa
wanachama wengi bado wanajua sheria za zamani ila sheria mpya
ya mfuko huo hawaijui ila wahusika wa mfuko huo wa NSSF wamekuwa
wakikaa kimya .
“Mfuko
wa NSSF kweli unachangamoto nyingi kwa wanachama wake kwanza
hawana kadi za uanachama na waajiri wengi wanatumia sheria za
zamani kwa mfanyakazi anapoingia
kuwa mwanachama wa NSSF ila mfumo huo bado unamkwaza mwanachama …hivyo nawaomba
NSSF kuiga mfano wa SSRA katika kutoa elimu na kuwabana baadhi ya
maofisa wa NSSF ambao wamekuwa wakitoa lugha chafu kwa wanachama
wake”
Kwa
upande wake meneja wa NSSF mkoa wa Iringa Marko Magheke mbali ya
kupongeza jitihada za SSRA kwa kuwafikia wanachama wake bado
alisema kuwa si kweli kama NSSF imekuwa ikiwanyanyasa wanachama
wake na kuwa kikwazo kikubwa cha kutoa elimu kinasababishwa na
waajiri ambao wamekuwa hawataki wafanyakazi wao kupewa elimu na
zaidi maeneo ambayo elimu imetolewa basi ni kupitia vyama vya
wafanyakazi wenyewe .
Kwani
alisema ni vigumu kuwakusanya wafanyakazi katika kampuni husika
bila ya mwajiri kukubali kufanya hivyo na kuwa waajiri
wengi hawapendi kuona wafanyakazi wao wanajua haki zao juu ya mifuko
hiyo ya kijamii.
“
Sisi NSSF kazi yetu moja wapo ni kutoa elimu kwa wanachama ila
tatizo ni waajiri wenyewe ambao wamekuwa wakishindwa kutoa
ushirikiano kwa kuwatoa wafanyakazi wake katika uzalishaji kwa
nia ya kupewa semina”
Pia
alisema kuhusu lugha chafu kwa wateja yeye hajapata kufikishiwa
malalamiko na kuwa kila mfanyakazi wa NSSF ananembo inayoonyesha
jina lake hivyo kwa yule mteja atajibiwa vibaya ni vema kusoma
jina na kupeleka malalamiko yake kwa meneja.
Hata
hivyo aliwataka waajiri wote kuhakikisha wanafikisha michango
ya wanachama wao kwa wakati na kuwa mwajiri kutofikisha
michango hiyo ni kinyume na taratibu na NSSF inawez kuchukua hatua
kali dhidi yake.
Alisema
kumekuwepo na changamoto kubwa ya waajiri kutofikisha michango ya
wanachama na kuwa eneo moja wapo linalosumbua kwa waajiri wake
kutofikisha michango ya wanachama wake ni pamoja na vyombo vya
habari ambapo katika mkoa wa Iringa wadaiwa sugu ambao wamepata
kufikishwa mahakamani ni pamoja na kituo kimoja cha radio mjini
hapa na sekta nyingine mbili.
Sarah Kibonde Msika ni mkuu wa mawasiliano uhamasishaji wa mamlaka ya usimamizi
na udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii (SSRA) nchini alisema kuwa
lengo la kufika mkoani Iringa ni kuhamasisha wafanyakazi kuijua
mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii.
Kwani
lisema kuwa wakati takwimu zinaonyesha kuwa watanzania kama
milioni 45 na nguvu kazi kama milioni 22 ila wanachama waliojiunga na
mifuko hilo ni milioni 1.7 pekee hivyo lengo la SSRA ni kuona
wanachama wanaongezeka zaidi.
Aliitaja
mifuko hiyo ya hifadhi ya jamii kwa Tanzania bara kuwa ni mfuko
wa hifadhi ya jamii (NSSF),Mfuko wa pensheni wa PPF,mfuko wa
pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF),,mfuko wa
pensheni kwa wafanyakazi wa serikali (GEPF),mfuko wa Pensheni wa LAPF
na mfuko wa Taifa wa bima ya Afya (NHIF) na kuwa kila mtanzania
anapaswa kujiunga na moja kati ya mifuko hiyo.
Alisema kuwa mifuko hiyo sita inasimamiwa na SSRA na kuwa lengo ni kuona wanachama wake
wanaendelea kujiunga kwa wingi na kunufaika na mifuko hiyo.
Msika
alisema kuwa Hifadhi ya jamii ni haki ya kila mtu na hii
imeainishwa katika ibara ya 11(1)) ya katiba ya jamuhuri ya
Muungano WA Tanzania na sera ya Taifa ya Hifadhi ya jamii ya
mwaka 2003 na kuwa haki hiyo pia imeainishwa kwenye mkataba wa
kimataifa wa haki za binadamu wa mwaka 1948 pamoja na mikataba
ya shirika la kazi Duniani (ILO).
|
0 comments:
Post a Comment