Serikali ya Libya imesema kuwa mtoto
wa Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Saadi Gaddafi, ameondoshwa nchini
Niger hivi sasa anashikiliwa mjini Tripoli.
Saadi alitoroka baada ya baba yake, Kanali Muammar Gaddafi kuuawa wakati wa mapinduzi yaliyofanyika mwaka 2011 nchini Libya.
Anashutumiwa kuwafyatulia risasi
waandamanaji na anadaiwa kutekeleza uhalifu mwingine wakati wa utawala
wa baba yake, yeye alipokuwa Kiongozi wa vikosi maalum vya kijeshi.
Serikali ya Libya imetoa taarifa hiyo mapema siku ya alhamisi kuwa wamempokea akitokea Niger.
awali , Niger ilikataa ombi la Libya
ilipotaka imsafirishe Saadi, huku waziri wa sheria wa Niger akihofu kuwa
Saadi atahukumiwa adhabu ya kifo.
Chanzo bbcswahili
0 comments:
Post a Comment