.
Katika uchaguzi huo, Ridhiwani
aliongoza kwa kupata kura 758 na kuwabwaga wenzake watatu, aliyekuwa
Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega aliyepata kura 335, Ramadhani Maneno
(206) na Changwa Mohamed Mkwazu aliyepata kura 17.
Katika uchaguzi huo, wapiga kura walitarajiwa kuwa 1,363 lakini waliojitokeza ni 1,321. Kura tano ziliharibika.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Saidi Bwanamdogo
kilichotokea Januari 22, mwaka huu.
Matokeo hayo yalitangazwa na Msimamizi
Msaidizi wa uchaguzi huo, Mjumbe Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC),
Rugemalila Rutatina katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Msata.
Akizungumza baada ya kutangazwa
mshindi, Ridhiwani alisema ushindi alioupata si wa kwake binafsi, bali
wa chama hicho kinachoongozwa na Rais Kikwete.
Alisema baada ya kupatikana kwa
mwakilishi wa chama, makundi yote yanatakiwa kuvunjwa na kuunda moja la
ushindi, kwa kuwa kilichoongoza ni CCM na si Ridhiwani.
"Ndugu zangu nawashukuruni kwa ushindi
mlionipa, natambua walikuwapo marafiki zangu, ndugu zangu wa karibu
wakiwanadi wagombea wenzangu, lakini sasa nimepita mimi... nashauri
kambi zetu ziishie hapa uwanjani tukitoka hapa tuwe na lugha moja ya
kukinadi chama chetu," alisema.
Kwa upande wake Madega alikiri uchaguzi huo kuwa na mchuano mkali kutokana na majina makubwa ya wagombea alioshindana nao.
Aliwataka viongozi wa chama wasiwabeze
wagombea walioshindwa, akisema wanastahili heshima zote ili kuwapa
morali ya kushirikiana kutetea jimbo hilo katika uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika Aprili 6, 2014.
Maneno alisema ni wajibu wa wanachama
wa CCM kuchagua kiongozi wanayemuona anafaa kupeperusha bendera, hivyo
iliwataka waliokuwa wanamuunga mkono kuelekeza nguvu zao kwa Ridhiwani
Mkwazu aliwashukuru wapiga kura kwa uamuzi wao na kuahidi kuendelea kumuunga mkono Ridhiwani katika mchakato unaoendelea.
0 comments:
Post a Comment