Rais Vladimir Putin wa Urusi.
Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema
matukio yaliyomng'oa madarakani rais wa nchi hiyo Viktor Yanukovych
yanatokana na "ukiukaji wa katiba na uporaji wa madaraka kijeshi."
Amesema"wanamgambo" wameitumbukiza nchi hiyo katika "vurugu".
Bwana Putin amesema Bwana Yanukovych alikubali mambo yote yaliyotakiwa na upinzani.
Vikosi vya Urusi na Ukraine katika
jimbo la Crimea nchini Ukraine viko katika hali ya tahadhari, lakini
wasiwasi uliokuwa umetanda kuwa Urusi ingefanya shambulio la kijeshi
nchini Ukraine, kwa sasa umepungua.
Chanzo, bbcswahil
0 comments:
Post a Comment