Baadhi 
ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kampasi ya Mwalimu 
Nyerere wakiwa katika jengo la utawala wa chuo hicho.
Na Riziki Mashaka.
Dar es Salaam, 
kuchelewa kwa mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu hasa katika kampasi ya 
Mwalimu Nyerere ya chuo kikuu cha Dar es Salaam kumezua hali ya ndivyo 
sivyo kwani mpaka sasa idadi ya wanafunzi waliofika chuoni hapo ni ndogo
 ukilinganisha na idadi yao kamili.
Mpaka sasa wanafunzi wa chuo hicho 
bado hawajapewa hela zao za kujikimu, hali hiyo imepelekea wanafunzi 
wengi kutofika katika maeneo ya chuo kwa muda muafaka kwa kuwa wengi wao
 wanasumbuliwa na tatizo la fedha na matokeo yake kushindwa kumudu 
baadhi ya mahitaji muhimu, idadi kubwa ya wanafunzi wa chuo hicho 
hutumia fedha hiyo kujilipia ada na shughuli nyingine za kimaisha kama 
elimu, maradhi na mambo mengine muhimu hususan ni wale watoto wa 
wakulima.
Wanafunzi wa chuo hicho wakiwa katika Vimbweta katika moja ya eneo maarufu la kujisomea linalojulikana kwa jina la Mdegree.
eneo la 
jengo la Nkrumah halikuonekana kuwa na watu wengi kama ilivyo kawaida, 
hii ni kutokana na uchache wa wanafunzi waliofika chuoni hapo mpaka 
sasa.
idadi ya wanafunzi waliohudhuria 
katika kampasi ya Mwalimu Nyerere ni ndogo ukilinganisha na idadi kamili
 ya wanafunzi wa chuo hicho hivyo ofisi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha 
Dar es Salaam (DARUSO) bado inalifatilia suala hilo kwa makini ili 
kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanapewa hela zao ili waweze kuendelea 
na masomo yao.
Baadhi ya wanafunzi wakirudi katika hostel zao za Mabibo hostel.
chanzo mjengwa blog 











0 comments:
Post a Comment