PG4A0947
Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakitoka Bungeni Mjini Dodoma Machi 6, 2014 baada ya Bunge hilo kusitihwa  kwa muda kufuatia Sitofahamu iliyotokea. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A0963
Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Halima  Mdee akitafakari baada ya wenzake kuondoka bungeni wakati Bunge hilo lilipositishwa  kwa muda mjini Dodoma Machi 6, 2014 kufuatia sintofahamu iliyokea. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A0987
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd  (wapili kushoto) wakijadili jambo na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba baada ya Bunge hilo kusitishwa kwa  muda Machi 6,2014 kufuatia sintofahamu ilitokea. Kutoka kushoto ni Katibu wa Bunge Thomas Kashilillah, Waziri  wa Nchi,Ofisi ya  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohammed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Stephen Wasira,  Waziri wa Katiba na Sheria  wa Zanzibar,  Abubakar  Khamis Bakari  na Mwanasheria  Mkuu wa Tanzania, Frederick Werema. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A0997
 
bungepic_696d3.jpg
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge maalum La Katiba Mh Pandu Kificho Ameahirisha Semina ya kujadili Kanuni za Bunge Maalum la Katika Kutokana na Vuruguru,
Kutokana na Hali ya Kutokuelewana Kati ya Mbunge wa Jimbo la Simanjiro Mh Ole Sendeka Kutoleana maneno na Mbunge Mwenzake wakati Mbunge Huyo alipohoji kuhusu Kanuni hizo. Hivyo hali hio ilipelekea kuairishwa kwa bunge hilo maalum Dodoma.