Friday, 7 March 2014

ANGALIA AJALI YA DALADALA ILIVYOTOKEA FRELIMO MKOANI IRINGA


Abiria wakitoka kwenye gari hiyo baada ya kupinduka

Abiria wakisaidiwa na wasamaria wema kutoka kwenye gari hiyo

Wananchi wakiendelea kuwasaidia abiria hao ili kuwahishwa hospitalini kwa matibabu

Hapa abiria wengine wakijiokoa wenyewe kutoka kwenye gari hilo.





FRANK KIBIKI, IRINGA
ZAIDI ya watu kumi, wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Iringa, baada daladala waliyokuwa wakisafiria kutoka Frelimo kwenda Tumaini, mjini Iringa kuacha njia na kuanguka.
Ajali  hiyo imetokea mchana  majira ya saa saba mchana, baada ya gari hiyo kushindwa kupanda mlima, na badala yake kurudi nyuma kabla ya kutumbukia kwenye mto.
Mwitikio imewashuhudia wasamaria wema wakiokoa majeruhi waliokuwa wamepanda daladala hiyo yenye namba za usajili, T 106 ABP ambao wote wamekimbizwahospitali kwa ajili ya matibabu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo kwamba taarifa zaidi itatolewa baada ya uchunguzi kukamilika. 
Chanzo:http:mwitikio.blogspot.com

Related Posts:

0 comments: