Saturday, 15 February 2014

WAZIRI CHIKAWE AKUTANA NA MKURUGENZI WA MARIE STOPES NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZAN

_DSC0001
Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa kwanza kutoka kushoto  akifurahia jambo  na Mkurugenzi Mkazi wa Maria Stopes nchini Tanzania Ulla Muller aliyekaa katikati ambaye alimtembelea Waziri wa Mambo wa Ndani ya Nchi ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Waziri Chikawe  hivi karibuni kuiongoza Wizara hiyo.
_DSC0003
Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa kwanza kutoka kushoto  akifafanua jambo kuhusu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi  mbele ya  Mkurugenzi Mkazi wa Maria Stopes nchini Tanzania Ulla Muller aliyekaa katikati ambaye alimtembelea Waziri Chikawe  ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha baada ya Waziri Chikawe kuteuliwa hivi karibuni kuiongoza Wizara hiyo, Kulia ni Michael Holscher Mkurugenzi wa Kimataifa wa Program za Maria Stopes ambaye aliambatana na  Mkurugenzi Muller.
_DSC0026
Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa pili kutoka kushoto  akisikiliza utambulisho  wa Balozi wa China Nchini Tanzania wa tatu kutoka kushoto  LU Youqing baada ya Balozi huyo kumtembelea Waziri Chikawe Ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha , Utambulisho huo ulitolewa na Mjumbe kutoka Ubalozi wa China hapa nchini  wa kwanza kutoka kushoto.  _DSC0030
Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mathias Chikawe wa kwanza kutoka kushoto  akisikiliza jambo kutoka kwa Balozi wa China Nchini Tanzania wa tatu kutoka kushoto  LU Youqing baada ya Balozi huyo kumtembelea Waziri Chikawe Ofisini kwake leo kwa lengo la kujitambulisha.Hivi karibuni Rais Jakaya Mrisho Kikwete Alimteuwa Waziri Mathias Chikawe Kuiongoza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Related Posts:

0 comments: