LISTI za Wagombea wa Madaraja mbalimbli ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa England ambao watazoa Tuzo za PFA, Professional Footballers' Association, Chama cha Wachezaji Soka wa Kulipwa, zimetangazwa.
Wachezaji Watatu wa Vinara wa Ligi Kuu England, Leicester City, Jamie Vardy, Riyad Mahrez na N'Golo Kante wamoja kwenye Listi ya Mtu 6 ya Wagombea wa Tuzo kuu.
Pamoja nao yupo Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil, Kiungo wa West Ham Dimitri Payet Straika wa Tottenham Harry Kane.
Kane pia yupo kwenye Listi nyingine ya wale wanaogombea kwa upande wa Vijana Tuzo ambayo aliitwaa Mwaka Jana.
Pamoja Kane kwenye Listi hiyo yupo mwenzake wa Tottenham Dele Alli. Tottenham
Washindi wa Tuzo hizi watatangazwa hapo Aprili 24.
Eden Hazard wa Chelsea ndie alietwaa Tuzo Kuu ya PFA Mwaka Jana.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
FAHAMU:
-Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa England wa PFA, yaani The Professional Footballers' Association Players' Player of the Year, hutolewa kila Mwaka kwa Mchezaji ambae ndie alikuwa Bora kwa Mwaka mzima huko England.
-Tuzo hii ilianzishwa Msimu wa 1973/74 na Mshindi kwa Kura za Wanachama wa PFA.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++
LISTI ZA WAGOMBEA:
-WANAUME:
-Dimitri Payet (West Ham)
-Harry Kane (Tottenham)
-Jamie Vardy (Leicester)
-Mesut Ozil (Arsenal)
-N'Golo Kante (Leicester)
-Riyad Mahrez (Leicester)
-VIJANA:
-Dele Alli (Tottenham)
-Harry Kane (Tottenham)
-Jack Butland (Stoke)
-Philippe Coutinho (Liverpool)
-Romelu Lukaku (Everton)
-Ross Barkley (Everton)
-WANAWAKE:
-Beth Mead (Sunderland)
-Gemma Davison (Chelsea)
-Hedvig Lindahl (Chelsea)
-Izzy Christiansen (Manchester City)
-Ji So-Yun (Chelsea)
#KIJANA KWA WANAWAKE:
-Beth Mead (Sunderland)
-Danielle Carter (Arsenal)
-Hannah Blundell (Chelsea)
-Keira Walsh (Manchester City)
-Nikita Parris (Manchester City)
0 comments:
Post a Comment