Thursday, 14 April 2016

Golikipa mrundi amefungiwa mechi nne kwenye Ligii kuu ya DR Congo

 G
olikipa wazamani wa klabu Vitalo FC na Prince Louis kutoka Burundi, Ndikumana Justin kabengele ambaye anaichezea klabu O C Muungano ya DR Congo amekumbwa na matatizo ya kufungiwa mechi nne na klabu yake kunyanganywa pointi zote ambazo mchezaji huu Justin ameshiriki.

Shirika la mpira wa Miguu nchini DR Congo imemshtumu mchezaji Justin kwa kosa la kutumia jina mbili tofauti, ila shutma izo klabu yake OC Muungano inaitupilia mbali na kujitetea kuwa ni makosa ya Shirika la Mpira kuandika jina la mchezaji wao wanavyo taka.
 Kesi yenyewe ni kuwa mchezaji Justin Ndikumana mwaka jana ametumia jina la ''Justin Ndikumana Kab'', halipo dai kuwa jina lake ni ''Justin Ndikumana Kabengele'' sio Kab amejibiwa kuwa wameamua kuifupisha kwajili jina lake ni ndefu.

 Huu mwaka wakati timu zote zimetakiwa kuwa na lecence mpya mpya, jina lake limefupishwa tena kwa ''Justin Ndik Kabengele'' ; baada ya uchunguzi na kugunduwa kuwa ni jina mbili tofauti ndio sababu ya kutowa adhabu ya kumuweka nje ya uwanja mechi nne na klabu yake kunyanganywa pointi zote ambazo mchezaji Justin Ndikumana ameshiriki.
Tuwakumbushe kuwa klabu ya mchezaji Justin Ndikumana ambaye ndiye golikipa namba moja wa klabu OC Muungano imewahi kuicharaza vibaya klabu babe nchini hapo DCMP kwa bao mbili bila (2-0) kwa baati mbaya ushindi uyo umeporwa na kuipa kama zawadi klabu ya DCMP.
Tayari klabu hii  OC Muungano ya hapo Bukavu nchini DR Congo imekwisha peleka malalamiko zao kwenye ngazi za juu la Shirika la Mpira ya DR Congo.

0 comments: