Mkurugenzi wa halmashauri  wa mji Kahama amepewa siku tisini awe amenunua mashine ya mionzi (x ray) kwa ajili ya hospitali ya mji Kahama.
Agizo hilo amepewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na  Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea hospitali hiyo pamoja na kuongea na watumishi wa kada ya afya wa mji huo.
Waziri Ummy alisema ametoa agizo hili ili kuweza  kurahisisha usumbufu wanaoupata wananchi wa wilaya hiyo kwa kwenda kupata huduma  nje ya hospitali ambapo wakati mwingine vipimo hivyo vinakuwa havisomeki vizuri kwa kukosa viwango vinavyostahili za mashine hizo.
Hata hivyo Waziri Ummy alisema upatikanaji wa mashine hizo itapunguza malalamiko mengi toka kwa wananchi kwa ukosefu wa kifaa tiba hicho ili  kwani hospitali hiyo hivi sasa inahudumia wananchi zaidi ya milioni moja hususani toka wilaya zote za mkoa huu.
Aidha, alizitaka halmashauri zote mjini kuweza kuwekeza kwenye huduma za vifaa tiba  ambavyo inarahisisha kugundua  matatizo yanayowakabili wananchi wanaofika kwenye kupata huduma na hivyo kuwapatia matibabu stahili wagonjwa wanaofika kupata matibabu kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.
“Siku hizi lazima muwekeze  kwenye kununua vifaa tiba ili kuweza kupata kutoa huduma nzuri, pesa mnakusanya na kahama ni halmashauri tajiri, mkurugenzi  nakupa siku tisini uwe umenunua mashine hiyo,” alisema Waziri Mwalimu.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Vita Kawawa amemuahidi waziri huyo kwamba amepokea maagizo yote aliyoyatoa na atayafuatilia ili kuweza kutatua malalamiko ya wananchi na yale ya watumishi wa kada ya afya.
Na Catherine Sungura, Kahama
1f14adf2-ca8b-40b0-a385-615cc362a552
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia kifaa cha kutengenezea maji tiba kwenye.hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
063472fe-1259-4dc3-b282-299df2e75bdd
Mfamasia mkuu wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, Luciano Lodrick akimpatia maelezo waziri wake wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto jinsi ya utengenezaji wa maji tiba.
aa2c0b91-5fee-43c8-bd35-17ebd8c0fbf6
Waziri Ummy Mwalimu akitoa galvanize kwa wagonjwa waliofika kupata matibabu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
c36d4347-1aac-44af-b203-060c97fb03c7
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wakazi wa Kahama waliofika hospitalini hapo kuangalia wagonjwa wao.
edb755e4-6ede-404a-9793-4e61eeb95699
Mh. Ummy Mwalimu akiangalia matangazo yaliyobandikwa kwenye ubao hospitalini hapo. Waziri Ummy ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kubandika gharama za matibabu pamoja na namba za simu kwa ajili ya kupokelea maoni na malalamiko toka kwa wananchi.
f8470464-fde8-48ff-b44f-fa84ba1836fc
Mh. Ummy Mwalimu akiwaelekeza Kamati ya Afya ya wilaya ya Kahama mahali linapotakiwa kuwekwa bango linaonesha huduma za wazee inapopatikana.
64ca7276-b88c-40d5-a953-fd89b7cc053b
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mh. Vita Kawawa (katikati) akionesha kwa vitendo bango hilo linapotakiwa kuwekwa, kushoto ni Mh.Ummy Mwalimu na kulia ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji kahama Anderson Msumba.