Dodoma. Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge imeipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutenga fedha ya kununulia bajaji na pikipiki zitakazotumiwa na watumishi kwa mwaka huu wa fedha, ikiwa ni mkakati wa kubana matumizi.
Wizara iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ni ya Sera, Bunge, Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu.
Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kwa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ya mwaka 2016/17, mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamed Mchengerwa amesema uamuzi wa namna hiyo unaendana na dhana ya kubana matumizi ya fedha ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Hata hivyo, hotuba ya bajeti iliyosomwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, haionyeshi pikipiki na bajaji hizo zinanuliwa kwa ajili ya wafanyakazi wa kada gani.
0 comments:
Post a Comment