Thursday, 21 April 2016

UKAWA Yazidi Kuitesa CCM ..Huyu Ndio Naibu Meya Mpya wa Jiji la Dar

 
Diwani  wa Kata ya Kiwalani, Mussa Kafana (Cuf), ameibuka mshindi katika uchaguzi wa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kwa kumbwaga mpinzani wake kwa kura nne.

Uchaguzi huo ulifanyika jana katika ukumbi wa Karimjee, baada ya madiwani wa jiji hilo, ambao pia ni wajumbe wa Baraza la Halmashauri ya jiji hilo kuapishwa.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa jiji hilo, Sarah Yohana alisema, Kafana ameibuka mshindi kwa kura 10 huku mpinzani wake Mariam Lulida (CCM) akipata kura sita. 

“Kura zilizopigwa ni 16 na hakuna iliyoharibika. Namtangaza Mussa Kafana kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam,” alisema Yohana. 

Awali Meya wa jiji hilo, Isaya Mwita alisema, baraza hilo lina jukumu la kuhakikisha linatekeleza majukumu yake ipasavyo na kila mjumbe kupitia chama chake anapaswa kutoa mchango utakaoweza kulibadilisha Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Kafana aliwashukuru wajumbe wa baraza hilo huku akiahidi kushirikiana nao bila kubagua itikadi za vyama vyao, kwani wanafanya kazi kwa ajili ya wananchi na si vyama vyao. 

Alisema kwa sasa vyama havina nafasi bali maendeleo ya wananchi wa jiji hilo ndio muhimu.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Huduma za Sheria kutoka Ofisi ya Rais, Tamisemi, Eustard Ngate, alisema, Halmashauri ya jiji hilo ilishawahi kuvunjika mara mbili mwaka 1983 na mwaka 1996 kutokana na viongozi wake kushindwa kuwajibika hivyo hawategemei hilo litokee

0 comments: