Naibu Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amewasilisha bungeni bajeti ya wizara yake bungeni na kupitishwa na wabunge wengine.
Naibu Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akiingia ukumbi wa Bunge siku ya kupitishwa bajeti ya Wizara hiyo mwishoni wa wiki mjini Dodoma.
Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akitoa hoja ili Bunge liidhinishe na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 ya Wizara hiyo mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa nchini, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akijibu hoja zilizoelekezwa na Wabunge kwenye Wizara hiyo kabla Bunge kuidhinisha na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki akitoa hoja ili Bunge liidhinishe na kupitisha bajeti ya Wizara hiyo ya mwaka 2016/2017.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu fedha za Serikali wakati wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora ya mwaka 2016/2017.
Wabunge wakiendelea na kikao cha Bunge cha bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora ya mwaka 2016/2017.
Wabunge wakiwapongeza Mawaziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utumishi na Utawala Bora baada Bunge kupisha bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2016/2017.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (kulia) akiongea na Wabunge Joseph Haule (wa kwanza kushoto) wa jimbo la Mikumi na Frank George Mwakajoka (katikati) wa jimbo laTunduma baada kikao cha Bunge mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (wa pili kushoto) akiongea na baadhi ya Wabunge mara baada ya kumaliza kikao cha Bunge mwishoni mwa wiki mjini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Mkoani Manyara Jitu Vrajlal Son.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) akiongea na baadhi ya Wabunge mara baada ya kumaliza kikao cha Bunge mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)
0 comments:
Post a Comment