Wednesday, 13 April 2016

TCRA kuwa tia mbaroni Lulu na Masogange Kwa Kuvaa Nguo Fupi na Kupost Mtandaoni

DAR ES SALAAM: Kufuatia tabia ya akina dada wengi kuweka picha za nusu utupu katika akaunti zao kwenye mitandao ya kijamii, wakiwemo mastaa kama Lulu, Masogange na wengineo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewapa kibano kikali, Risasi Mchanganyiko lina stori kamili.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungi alisema ingawa jukumu la kuwakamata wote wanaoweka picha zinazokiuka maadili ni la jeshi la polisi kupitia kitengo cha makosa ya mtandao (Cyber Crime), taasisi hiyo inawasiliana na wamiliki wa mitandao ya kijamii ili kutafuta namna nzuri ya kuwadhibiti.

“Tunachofanya ni kuzungumza na hawa watu ili kuwafungia wote wanaokiuka maadili, tunajua baadhi yao wanajiunga katika mitandao kwa kutumia majina ya uongo, lakini sisi tutazifungia ‘line’ maana kila moja ina namba zake za siri na hazifanani na zingine, hivyo ukiondolewa kwa kufungiwa huwezi tena kujiunga kwa vile kule kwenye mitandao wanatambua namba,” alisema.
Akifafanua, Mungi alisema wakifikia makubaliano na mitandao hiyo ya kijamii aliyoitaja kuwa ni pamoja na Twitter, Facebook, Instagram, Badoo, Snapchat na mingineyo, mtu anayeweka picha zinazokiuka maadili atafungiwa na hataweza kujiunga tena hata abadili jina mara ngapi.

Katika mitandao hiyo, baadhi ya wasichana wakiwemo maarufu, wamekuwa wakiweka picha zinazokiuka maadili, kwa sababu mbalimbali wengine wakitajwa kuwa wanajiuza.
Baadhi wa wasichana wenye majina maarufu ambao wamekuwa wakitupia picha zenye utata mara kwa mara katika mitandao licha ya Lulu ni pamoja na Agnes Gerald ‘Masogange’, Gigy Money, Shilole, Kidoa, Anti Lulu, Isabela Mpanda na wengineo.

0 comments: