Saturday, 23 April 2016

Hali na Kuhusu Matibabu ya Chid Benz..yanaendeleaje toka Sober House


Kama unakumbuka March 22, 2016 meneja wa Diamond Platnumz, Babu Tale alimpeleka rapper Chid Benz Sober House iliyopo Bagamoyo iitwayo Life and Hope Rehabilitation Centre kwaajili ya kupata matibabu ya kuacha kutumia madawa ya kulevya na kurudi kwenye hali yake ya mwanzo.

Sasa hapa Ayo TV  imempata msanii wa Hip Hop, Kalapina ambaye hivi karibuni alikwenda Sober House ilipo Bagamoyo kumjulia hali Chid Benz..

‘Chid benz sasa hivi anaendelea vizuri ni tofauti na vile mwanzo alivyokuwa, inategemea na mtu alivyoathirika atakaa siku ngapi mtu anaweza anakaa miezi sita au miezi saba Chid Benz ana siku 29 inategemea pia na dawa gani anazopewa ili mwili urudi kama zamani’– Kalapina

Itazame hii video hapa Kalapina amezungumza mengi kuhusu matibabu ya Chid Benz


 

0 comments: