Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Dismas Kisusi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Mawemilu.
“Manyilizu alimkuta mdogo wake akifanya mapenzi na mkewe, alivyomuhoji, mdogo wake alichukua kitu akampiga nacho kichwani hivyo alifariki dunia wakati akiendelea na matibabu katika zahanati ya Kijiji cha Mawemilu,” alisema Kisusi.
Alidai mtuhumiwa na mwanamke walikimbia baada ya kufanya tukio hilo.
Katika tukio jingine, watu wawili wameuawa kwa kupigwa mawe na marungu kisha miili yao kuchomwa moto na wananchi.
Kisusi alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Kijiji cha Shimba wilayani Kahama.
Kisusi alisema watu hao walituhumiwa kuwa ni majambazi baada ya kumvamia Mchongaraji Ndalawa (65), akiwa amelala nyumbani kwake wakimtaka awape fedha.
“Alivyosema hana walimkata kwa panga kichwani, ndipo wananchi walijichukulia sheria mkononi kwa kuwaua,” alisema.
Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama na hali yake inaendelea vizuri.
0 comments:
Post a Comment