Sunday, 17 April 2016

SAKATA LA LUGUMI : Rais alisema ukitajwa kwa rushwa unaondoka hapo hapo hakuna kuunda tume

 
Wakati wa hotuba yake Mh Rais aliwahi kusema kua mtimishi wa umma akitajwa kwa ufisadi tayari ana doa atawajibishwa hapo hapo hakuna mambo kuunda tume.Sasa waziri kitwanga anatajwa sana kua na maslahi kwenye hili sakata, sasa kinachosubiriwa ni nini?


Uchunguzi Mara nyingi ni kujiridhisha na uhusika wa mtu katika sakata flani ili kukwepa mishale ya kisheria maana kumshutumu mtu bila ushahidi mwisho wa Siku ataidai haki yake Mahakamani.Kuunda tume ni kuujua ukweli wa jambo na ikithibitika ni kweli basi mtu achukuliwe hatua za kisheri bila kumuonea haya mtu.

Waziri kitwanga akae pembeni kupisha uchunguzi maana kampuni zake zimetajwa na kuunganishwa na mnufaika mkuu kampuni ya LUGUMI.Ni swali la kijiuliza ni kwanini mtu anakua waziri katika wizara ambayo tayari anafanya biashara nayo? hivi hakuna mgongano wa kimaslahi hapa? Sheria ya maadili ya utumishi wa umma inasemaje? Kiukweli Kitwanga mpaka sasa kwa maoni yangu hatakiwi kua waziri wa mambo ya ndani,kama sivyo basi ni bora kumhamisha wizara.Kampuni zake kuhusishwa kufanya biashara ndani ya wizara hiyo tayari ni tatizo kwake.

Chanzo:Jamii Forums

0 comments: