Tuesday, 12 April 2016

Ma wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015CT yatangaza majina ya AJAT 2015


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MCT yatangaza majina ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015
·           Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Nyanduga kuwa Mgeni Rasmi

Kamati ya maandalizi ya EJAT 2015 leo limetangaza majina 84 ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015. Idadi hiyo ni ongezeko la wateule 31 ukilinganisha na tuzo za 2014 ambapo wateule walikuwa ni 53 tu.

Pia kamati imeeleza kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tom Bahame Nyanduga ndio Mgeni Rasmi kwenye Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT ) 2015  zitakazofanyika kwenye tamasha la usiku la utoaji wa tuzo hizo  Aprili 29, 2016 , Dar es Salaam.

Kutangazwa kwa wateule wa EJAT 2015 kunafuatia kukamilika kwa kazi ya kuzipitia na kuchagua zile zilizo na ubora zaidi iliyofanywa na jopo la majaji 10 lililokaa mwezi Machi mwaka huu. Majaji hao ambao ni wataalamu mbalimbali wa masuala ya habari walipitia kazi za kiandishi zaidi ya 570 zilizowasilishwa kwenye makundi ya kushindaniwa 22 kwenye tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2015.

Ripoti ya jopo la majaji hao kuhusu wateule wa EJAT 2015, inaonyesha kuwa  kumekuwa  na ongezeko kubwa kwa  wateule kwa upande wa luninga ambapo kuna wateule  27 kutoka wateule wawili katika tuzo za 2014. Pia kuna ongezeko kwenye wateule wa redio kutoka 17 hadi 27. Hata hivyo kwa upande wa magazeti wateule wamepungua kidogo kutoka wateule 34 wa tuzo za 2014 hadi 32 kwa tuzo za mwaka 2015.  


Idadi ya wateule wanawake pia imeongezeka kufikia 28 kutoka wateule 18 kwenye tuzo za EJAT 2014.  Pia ripoti inaonyesha kuongezeka kwa kazi zilizoletwa na redio za kijamii mwaka huu ambapo baadhi yao zimeweza kutoa wateule kwenye tuzo za EJAT 2015.

Jopo hilo la majaji liliongozwa na mwenyekiti wake, Bi. Valerie Msoka, wajumbe wengine walikuwa  Dk. Joyce Bazira Ntobi ambaye alikuwa katibu wa jopo, na Ali  Uki. Wanajopo wengine walikuwa Jesse  Kwayu, Kiondo Mshana,  Juma Dihule, Godfrey  Nago, Nathan Mpangala na  Pili Mtambalike. Waandishi hao 84 wataingia kwenye kinyang’anyiro cha mashindano ya EJAT 2015. 

Majaji hao 10 waliapishwa na Rais wa Baraza la Habari Tanzania, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo Machi  11, 2016 kabla ya kuanza kazi hiyo. Hii itakuwa ni  mara ya saba kuwatuza waandishi waliofanya vizuri katika kazi zao za kiuandishi chini ya utaratibu wa EJAT.

Sambamba na EJAT, Jopo la wataalam kwa ajili ya Tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Uandishi wa Habari (LAJA) umeanza kazi ya kutafuta mteule wa tuzo hiyo kwa mwaka huu ambae atatangazwa wakati wa Tamasha hilo la usiku.  Jopo la LAJA linalongozwa na Mwenyekiti wake Bi. Lilian Kallaghe lina wajumbe watano ambao ni pamoja na Hamis Mzee, Fili Karashani, Joseph Kulangwa na Wenceslaus Mushi.

Makundi yaliyoshindaniwa ni yafuatayo:

1. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchumi na Biashara
2. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Michezo na Utamaduni
3. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Mazingira
4. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya
5. Tuzo ya Uandishi wa Habari za VVU/Ukimwi
6. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watoto
7. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utawala Bora
8. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Jinsia
9. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi na Teknolojia
10 Tuzo ya Uandishi wa Habari za Uchunguzi
11. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ya Mama na Mtoto
12. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu
13. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Utalii na Uhifadhi
14. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Watu Wenye Ulemavu
15. Mpiga Picha Bora – Magazeti
16. Mpiga Picha Bora – Runinga
17. Mchora Katuni Bora
18. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kilimo
19. Tuzo ya Afya ya Uzazi kwa vijana
20. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini
21. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Manunuzi ya Umma
22. Tuzo ya Uandishi wa Habari za Kodi na Ukusanyaji Mapato

Ifuatayo ni orodha ya wateule wa EJAT 2015 ambao wanatoka kwenye vyombo mbalimbali vya habari








WATEULE WA EJAT 2015
SN
JINA LA MWANDISHI
CHOMBO CHA HABARI
MKOA ANAOTOKA

1.       
Sylvester Joseph
Afya Radio
Mwanza
2.       
Fatuma Mtengamani
Ulanga FM
Ulanga-Mahenge
(Morogoro)
3.       
Adam Hhando
CG FM
Tabora
4.       
Abisae Maeda
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
5.       
Mwashamba Juma
Zanzibar Leo
Zanzibar
6.       
Jackline Masinde
Mwananchi
DSM
7.       
Peter Rodgers
ITV
Mwanza
8.       
Lucas Maziku
Star TV
Mwanza
9.       
Maajabu Madiwa
Pangani FM
Pangani-Tanga
10.   
Ezekiel Kamanga
BBC & Bomba FM
Mbeya
11.   
Malongo Mbeho
Metro FM
Mwanza
12.   
Annastazia Maginga
Raia Tanzania
Mwanza
13.   
John Leon Lewanga            
TBC
DSM
14.   
Mussa Kinkaya
Sunrise FM
Arusha
15.   
Victor Makwawa
Dodoma FM
Dodoma
16.   
Pili Mlindwa
Pangani FM
Pangani-Tanga
17.   
Zulfa Golay

Mwananchi

Arusha
18.   
Tumaini Msowoya
Mwananchi
Iringa
19.   
Nuzulack Dausen
The Citizen

DSM
20.   
 Haji Mohamed
Zanzibar Leo
Pemba-Zanzibar
21.   
Silvano Kayera
Mlimani
DSM
22.   
Christian Msafiri
CG FM
Tabora
23.   
Grace Mbise
Bomba FM

Mbeya
24.   
Salome Kitomari
Nipashe
DSM
25.   
Kelvin Matandiko
Mwananchi
DSM
26.   
Mansour Jumanne
SAUT FM
Mwanza

27.   
Frank Bahati
TBC1
DSM
28.   
Khamis Suleiman
Channel Ten
DSM
29.   
Emmanuel Buhohela
ITV
DSM
30.   
Lusekelo Philemon
The Guardian
DSM
31.   
John Nsuza          
TV1
Arusha
32.   
Esther Zelamula
Channel ten
DSM
33.   
Elibahati Akyoo
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
Arusha
34.   
Idd Juma
Afya Radio
Mwanza
35.   
Mashaka Mgeta
The Guardian
DSM
36.   
Kisali Simba
Star TV
Shinyanga
37.   
Editha Kinyaiya
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
38.   
Emmanuel Kitomari
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
39.   
Maulid kambaya
Radio One
DSM
40.   
Lulu George
Nipashe
Tanga
41.   
Mussa Siwayombe
Mwananchi
Arusha
42.   
Victor Eliah
TBC
DSM
43.   
Cassius Mdami
Channel Ten
DSM
44.   
Anthony Masai
Triple A FM
Arusha
45.   
Temigunga Mahondo
Radio Country FM
Iringa
46.   
Beatrice Shayo
Nipashe
DSM
47.   
Rahma Suleiman
Nipashe
Zanzibar
48.   
Haika Kimaro
The Citizen
DSM
49.   
Halfan Lihundi
ITV
Arusha
50.   
Lydia Igarabuza
EATV
DSM
51.   
Valeria Mwalongo
Tumaini
DSM
52.   
Peninah Kajura
HHC Radio
Mwanza
53.   
Goodluck Mvamba
SAUT FM
Mwanza
54.   
Said Michael
Mtanzania
DSM
55.   
Abdul Kingo
Nipashe
DSM
56.   
Nora Damian
Mtanzania
DSM
57.   
Sauli Gilliard
The Citizen

DSM
58.   
Alfayo Misiyeki
TV1/Kilimanjaro Film Institute
Arusha
59.   
Samson Kapinga
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
Arusha
60.   
Florence Majani
Mwananchi

DSM
61.   
Selemani Mkufya
TBC1
DSM
62.   
Kasilda Mgeni
Star TV
Morogoro
63.   
Tuma Dandi
Mlimani
DSM
64.   
Eveline Mhozya
CG FM
Tabora
65.   
Vivian Pyuza
CG FM
Tabora
66.   
Joseph Mwendapole
Nipashe
DSM
67.   
Hadija Jumanne
Mwananchi
DSM
68.   
Christina Mwakangale
Nipashe

DSM
69.   
Sanula Athanas
Nipashe
DSM
70.   
Mwanahiba Richard
Mwanaspoti
DSM
71.   
Japhary Ramadhan
ABM FM
Dodoma
72.   
Bernard Lugongo
The Citizen
DSM
73.   
Emmanuel Mollel
TV1/ Kilimanjaro Film Institute
Arusha
74.   
Joel Ulomi
Arusha One
Arusha
75.   
Haji Nassor

Zanzibar Leo

Chake Chake-Pemba
76.   
Peti Siyame
Habari Leo
Sumbawanga-Rukwa
77.   
Robert Okanda
Dailynews
DSM

78.   
Nuru Hassan
Afya
Mwanza
79.   
Shija Felician
The Citizen
Kahama
80.   
Salum Maige
Mwananchi
Geita
81.   
Projestus Binamungu
Star TV
Mwanza
82.   
Regina Kulindwa
Afya
Mwanza
83.   
Denis Nyali

Nuru
Iringa
84.   
Sam Mahela
ITV
DSM


Waandaaji wa EJAT 2015 ni pamoja na Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika- Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Jukwaa la Wahariri (TEF), Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (MOAT), Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Chama cha Waandishi wa Habari Walio katika Mapambano Dhidi ya UKIMWI Tanzania (AJAAT), Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), PSI-Tanzania, Unicef, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Haki Elimu, SIKIKA, Evidence for Action, Amref Health Africa na BESTDialogue/ANSAF.




Kajubi D. Mukajanga 
Mwenyekiti

Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2015

0 comments: