Tuesday, 11 February 2014

WAKAZI WA KATA YA MBUGANI WALILIA UMEME

index

Mahmoud Ahmad
Wakazi wa kata ya mbugani mtaa wa mabatini kaskazini eneo la mwembe giza wamekiomba chama cha  mapinduzi  katika kata hiyo na wafadhili mbalimbali hapa nchini kuwasaidia mchango wa hali na mali katika kufanikisha upatikanaji wa huduma ya umeme kwenye eneo lao kwa kuwasaidia mchango wa kupata nguzo tano kati ya saba zinazohitajika.
Wakiongea kwenye kikao chao cha ukusanyaji wa michango ya kupata huduma hiyo ya umeme mbele ya katibu wa ccm wa kata hiyo Gerald Mashala wakazi hao wamemuelezea kuwa wamejitahidi kukusanya fedha za kununulia nguzo mbili hadi sasa lakini kutokana kipato chao kuwa kidogo wanakiomba chama cha mapinduzi kuwasaidia upatikanaji wa nguzo tano iliwaweze kusogeza huduma hiyo.
Pia wakawataka wafadhili mbalimbali kusaidia upatikanaji  wa hizo nguzo tano za umeme ilikuweza kupata urahisi wa ufikaji wa eneo hilo kwani kwa kipindi hichi wazee,wagonjwa na walemavu wamekuwa wakipata tabu kutokana na giza na ufikaji wa eneo lao kwani lipo milimani.
“Unajua ndugu mwandishi eneo letu lipo milimani na tunaishi na wazee,walemavu na saa zingine wagonjwa na wajawazito kwa hali hii ni hatari kubwa sana nyakati za usiku ufikaji wakeunakuwa wa shida hivyo kupitia wewe tunaomba kupatwa huduma hiyo kwa haraka”alisisitiza Peter.
Hata hivyo CCM kata hiyo imeahidi kutoa kiasi cha sh.200,000 katika jitihada za kufanikisha juhudi za kujiletea maendeleo kwani wameonyesha juhudi kubwa na hiyo ni kusaidia ilani ya chama hicho kufikisha asilimia 30%wawewamefikishiwa huduma ya umeme kwwa nchi nzima.
Mashalla pia akasema atasaidia kwenda wafadhili mbalimbali wenye moyo wa kusaidia maendeleo ilikuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo huku akiyaomba makampuni mbalimbali kusaidia kwa karibu jamii za pembezoni ilikuweza kujiona hawajatengwa na jamii.
“Unajua wakazi hawa ni sehemu ya wakazi wa kata hii wanaohitaji huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma hii ya umeme na maji kwani limekkuwa ni tatizo sugu huku mamlaka husika zikishindwa kukaa na jamii kujua zitasaidiaje na hili ni tatizo”alisema mashalla.

Related Posts:

0 comments: