Athari mbaya itokanayo na vikwavo vya
upande mmoja vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
vimelalamikiwa vikali na viongozi wa Afrika Kusini. Naibu Katibu Mkuu wa
Idara ya Mambo ya Asia na Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi
hiyo, sambamba na kusema kuwa Iran imepiga hatua kubwa katika teknlojia
za kisasa na viwanda vya madawa amesema kuwa, maendeleo ya Iran katika
nyuga za elimu na teknolijia, hususan katika masuala ya nyuklia,
yanakwenda kwa kasi sana. Amesema kuwa, walimwengu wamekubali kwamba,
kufanya mazungumzo na Iran ni kwa manufaa ya pande zinazofanya
mazungumzo hayo. Itakumbukwa kuwa, Waziri wa Mambo ya Nje ya Afrika
Kusini, Bi Maite Nkoana-Mashabane hivi karibuni alisema
kuwa nchi yake iko tayari kuanza
kununua mafuta ghafi kutoka Iran na kuongeza kuwa, vikwazo vilivyowekwa
dhidi ya Tehran, vimekuwa na taathira mbaya kwa uchumi kwa nchi
mbalimbali za dunia. Mashabane amesisitiza kuwa, kuna udharura wa
kuondolewa vikwazo hivyo visivyo na msingi kwa ajili ya maslahi ya
walimwengu. Amesisitiza kuwa, viwanda kadhaa nchini Afrika Kusini
vimepata hasara kubwa katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na
kuzuiliwa kununua mafuta ya Iran.
Chanzo, kiswahili.irib.ir/habari
Chanzo, kiswahili.irib.ir/habari
0 comments:
Post a Comment