Tuesday, 3 December 2013

FIFA YATOA MWONGOZO WA DROO YA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA!

RASMI ZAPANGWA KWENYE VYUNGU VYA DROO!
BRAZIL_2014_ORIJINO11FIFA leo imetangaza mwongozo wa jinsi Droo ya kupanga Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil kuanzia Juni 12 Mwakani zitakavyofanyika.
Fainali hizo zenye Nchi 32 zitapangwa katika Makundi 8 ya Timu 4 kila moja.
Katika mwongozo huo, FIFA imesema Timu 8 za juu kwa Ubora Duniani [Kwa mujibu wa Listi iliyotoka Oktoba], pamoja na Wenyeji Brazil, zipo Chungu Namba 1 na zitapangwa kuanzia Kundi A hadi H ili kuzitenganisha.
Brazil, kama Wenyeji, tayari wamewekwa Kundi A na watacheza Mechi ya Ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia hapo Juni 12 huko Sao Paulo.
-CHUNGU NAMBA 1: Brazil, Spain, Argentina, Belgium, Colombia, Germany, Switzerland, Uruguay
-CHUNGU NAMBA 2: Ivory Coast, Ghana, Algeria, Nigeria, Cameroon, Chile, Ecuador
-CHUNGU NAMBA 3: Japan, Iran, South Korea, Australia, United States, Mexico, Costa Rica, Honduras
-CHUNGU NAMBA 4: Bosnia, Croatia, England, Greece, Italy, Netherlands, Portugal, Russia, France
FAHAMU: Kabla Droo kufanyika itafanyika Droo maalum kuihamisha moja ya Timu za Ulaya toka Chungu Namba 4 na kuiweka Namba 2 ili kuleta uwiano wa Nchi toka Mabara tofauti.
Pia, Timu 4 za kutoka Marekani ya Kusini, Brazil, Uruguay, Colombia na Argentina zitawekwa kwa muda Chungu Namba X. Timu 3 ambazo hazitapangiwa ile Timu ya Ulaya ambayo ilipelekwa Chungu Namba 2 zitarudishwa kwenye Droo kubwa kama walivyopangiwa awali.

0 comments: