Jumamosi Februari 15
Rhino Rangs v Mgambo JKT
Ashanti United v Kagera Sugar
Mtibwa Sugar v Tanzania Prisons
JKT Oljoro v JKT Ruvu
Mbeya City v Simba
Ruvu Shooting v Coastal Union

UWANJA
wa Sokoine huko Jijini Mbeya, Jumamosi Hii ya leo kunatarajiwa kuwaka moto kwa
pambano kali la VPL, Ligi Kuu Vodacom, ambapo Wenyeji Mbeya City
wanawania ushindi dhidi ya Simba ili kutwaa uongozi wa Ligi hiyo.
Mbeya City, ambao wako Nafasi ya Tatu,
wakiifunga Simba watazipiku Yanga na Azam FC na kutwaa nafasi ya kwanza
na Simba nao wakishinda watafikia Pointi 34 sawa na Mbeya City lakini
wataipiku na wao kushika Nafasi ya Tatu kwa ubora wa Magoli.
Wikiendi hii, Azam FC, ambao ndio
wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 36, na Timu ya Pili, Yanga, wenye
Pointi 35, hawachezi kwa vile wako nje ya Nchi kucheza Mechi zao za
Marudiano za Michuano ya Klabu Barani Afrika.
Azam FC wako huko Beira, Nchini Msumbiji
kurudiana na Ferroviario da Beira huku wao wakiwa wameshinda Bao 1-0
walipocheza Dar es Salaam wakati Yanga wako Visiwa vya Comoro kurudiana
na Komorozine de Domoni ambayo waliipiga 7-0 Jijini Dar es Salaam.
Mechi zinazofuata kwa Azam FC na Yanga
ni hapo Februari 22 wakati Yanga watakapocheza na Ruvu Shooting na Azam
FC kukutana na Tanzania Prisons.
Mbali ya Mechi ya Mbeya City na Simba, hiyo LEO zipo Mechi nyingine 5 za Ligi.
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
GD |
PTS |
1 |
Azam FC |
16 |
10 |
6 |
0 |
19 |
36 |
2 |
Yanga SC |
16 |
10 |
5 |
1 |
22 |
35 |
3 |
Mbeya City |
17 |
9 |
7 |
1 |
10 |
34 |
4 |
Simba SC |
17 |
8 |
7 |
2 |
17 |
31 |
5 |
Coastal Union |
17 |
4 |
10 |
3 |
4 |
22 |
6 |
Ruvu Shooting |
16 |
5 |
7 |
4 |
2 |
22 |
7 |
Mtibwa Sugar |
17 |
5 |
7 |
5 |
0 |
22 |
8 |
Kagera Sugar |
17 |
5 |
7 |
5 |
0 |
22 |
9 |
JKT Ruvu |
16 |
6 |
0 |
10 |
-8 |
18 |
10 |
Ashanti UTD |
16 |
3 |
4 |
9 |
-14 |
13 |
11 |
JKT Oljoro |
17 |
2 |
7 |
8 |
-14 |
13 |
12 |
Mgambo |
17 |
3 |
4 |
10 |
-18 |
13 |
13 |
Rhino Rangers |
17 |
2 |
6 |
9 |
-10 |
12 |
14 |
Prisons FC |
14 |
1 |
7 |
6 |
-10 |
10 |
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Februari 19
Tanzania Prisons v JKT Ruvu
Jumamosi Februari 22
Ruvu Shooting v Yanga
Kagera Sugar v Rhino Rangers
Mtibwa Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Mbeya City
JKT Oljoro v Mgambo JKT
Azam FC v Tanzania Prisons
Jumapili Februari 23
Simba v JKT Ruvu
0 comments:
Post a Comment