TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 14, 2014
TWIGA STARS YALALA 2-1 ZAMBIA
Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga timu hizo zilikuwa suluhu.
Wenyeji ndiyo walianza kupata bao
lililofungwa na Hellen Mubanga dakika ya 75. Mfungaji huyo aliyeingia
kipindi cha pili nchini alimalizia wavuni mpira uliotemwa na kipa Fatuma
Omari.
Dakika nne baadaye Zambia ambao walikuwa
wakishangiliwa kwa nguvu na washabiki wao baada ya kufunga la kwanza,
walipata bao la pili ambalo nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili
alijifunga mwenyewe.
Mwasikili alikuwa akijaribu kutoa nje
mpira uliopigwa na nahodha wa Shepolopolo, Mupopo Kabange ambapo
ulipishana na kipa Fatuma Omari kabla ya kujaa wavuni.
Bao la Twiga Stars lilifungwa na Donisia
Daniel dakika ya 90. Beki huyo wa kushoto ambaye pia ni mchezaji wa
Tanzanite alipanda mbele kuongeza mashambulizi ambapo akiwa nje ya eneo
la hatari alipiga shuti lililomshinda kipa Hazel Nali.
Akizungumza baada ya mechi, Kocha wa
Twiga Stars, Rogasian Kaijage alisema amebaini upungufu katika kikosi
chake ambao ataufanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano ili timu yake
iweze kusonga mbele.
“Kwa matokeo haya bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano nyumbani na kusonga mbele,” alisema Kaijage.
Twiga Stars iliwakilishwa na Fatuma
Omari, Fatuma Bashiru, Donisia Daniel, Fatuma Issa, Evelyn Sekikubo,
Sophia Mwasikili, Vumilia Maarifa, Mwapewa Mtumwa/Amina Ali, Asha
Rashid, Etoe Mlenzi/Zena Khamis na Shelida Boniface.
Timu hiyo inarejea nyumbani kesho kwa
ndege ya Fastjet ambapo itatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Lusaka, Zambia
0 comments:
Post a Comment