Saturday, 15 February 2014

MANCHESTER CITY NA CHELSEA KUKUTANA TENA LEO FA CUP

city_bd2b8.jpg >>JUMAPILI NI ARSENAL v LIVERPOOL!!
>>NANI KUTINGA ROBO FAINALI??

FA CUP
Raundi ya Tano
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 15
1545 Sunderland v Southampton
1800 Cardiff v Wigan
1800 Sheff Wed v Charlton
2015 Man City v Chelsea
Jumapili Februari 16
1630 Everton v Swansea
1800 Sheff Utd v Nottm Forest
1900 Arsenal v Liverpool
Jumatatu Februari 17
2245 Brighton v Hull

Gumzo kubwa kwa Mechi hizi za FA CUP ni zile Bigi Mechi mbili ambapo Jumamosi, huko Etihad, Manchester City wataikaribisha Chelsea huku wakikumbuka kufungwa na Chelsea Bao 1-0 Wiki iliyopita kwenye Mechi ya Ligi na Jumapili, ndani ya Emirates, Arsenal, watawaalika Liverpool ambao Jumamosi iliyopita waliinyuka Arsenal 5-1 huko Anfield kwenye Mechi ya Ligi.
Mechi nyingine ambazo zitakutanisha Timu za Ligi Kuu pekee ni zile za Sunderland v Southampton na Everton v Swansea.
ZIFUATAZO NI DONDOO ZA MECHI ZOTE NANE:
SUNDERLAND v SOUTHAMPTON
Timu hizi zimewahi kukutana kwenye FA CUP mara 7 na mara 5 Sunderland kufuzu.
Sunderland wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa wameshinda Mechi 6 na kufungwa 2 katika Mechi zao 9 zilizopita na Winga wao, Adam Johnson, akiwa amefunga Bao 7 katika Mechi 8.
Southampton wao hawajafungwa katika Mechi zao 8 zilizopita wakiwa wameshinda 5 na Sare 3.
CARDIFF CITY v WIGAN ATHLETIC
Timu hizi hazijawahi kukutana kwenye FA CUP.
Kwenye Ligi, Timu hizi zimekutana mara 10 na Cardiff City hawajashinda hata mara moja baada Kufungwa 5 na Sare 5.
Wigan ndio Mabingwa Watetezi wa FA CUP na ni Timu ya kwanza kutwaa Kombe hilo na kuporomoka Daraja Msimu huo huo ambapo Msimu uliopita walishushwa kutoka Ligi Kuu kwenda Championship.
SHEFFIELD WEDNESDAY v CHARLTON ATHLETIC
Wameshawahi kukutana mara 3 kwenye FA CUP, zote zikiwa kwenye Raundi ya Tatu, Miaka ya 1976, 1996, 2006, na zote walishinda Charlton.
Meneja wa sasa wa Charlton, Chris Powell, aliichezea Klabu hiyo hiyo walipokutana na Sheffield mara ya mwisho kwenye FA CUP, Mwaka 2006, na kushinda 4-2.
MANCHESTER CITY v CHELSEA
Wiki iliyopita, kwenye Mechi ya Ligi iliyochezwa Etihad, Chelsea waliifunga Man City Bao 1-0 na kwenye FA CUP wameshakutana mara 4 na City kufungwa mara ya kwanza, Mwaka 1915, lakini wameshinda mara zote 3 zilizobakia ikiwemo mara ya mwisho Msimu uliopita walipoifunga Chelsea 2-1 kwenye Nusu Fainali.
Man City hawajashinda katika Mechi zao mbili zilizopita, wakifungwa moja na Sare moja, lakini Chelsea hawajafungwa katika Mechi zao 12 zilizopita wakishinda 9 na Sare 3.
EVERTON v SWANSEA CITY
Wameshakutana mara moja tu kwenye FA CUP, Mwaka 1954, na Everton kushinda Bao 3-0.
Everton wameshinda Mechi 6 kati ya 7 walizocheza mwisho Uwanjani kwao Goodison Park huku Swansea wakishinda Mechi 2 tu ya 10 walizocheza mwisho Ugenini.
SHEFFIELD UNITED v NOTTINGHAM FOREST
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Timu hizi kukutana baada ya kuvuka Raundi ya Nne ya FA CUP na Sheffield United kuifunga Nottingham Fores 3-0 kwenye Raundi ya Sita Mwaka 1928.
Sheffield United hawajafungwa wakiwa kwao Bramall Lane katika Mechi 7 zilizopita wakishinda 3 na Sare 4 lakini Nottingham Forest hawajafungwa hata Mechi moja tangu Tarehe 29 Novemba 2013 wakishinda Mechi 9 na Sare 7.
ARSENAL v LIVERPOOL
Ni FA CUP lakini Arsenal watataka kulipa kisasi cha Jumamosi iliyopita kunyukwa Bao 5-1 huko Anfield kwenye Mechi ya Ligi.
Kwenye FA CUP, Timu hizi zimekuwa zikukutana kila Msimu katika Misimu 12 iliyopita na Arsenal kushinda mara 7, zikiwemo Fainali 2, na Liverpool  kushinda Fainali 1 na kusonga mara 4 mbele ya Arsenal.
Katika Mechi za FA CUP 8 zilizopita , Arsenal wamefungwa moja tu na Liverpool na hiyo ilikuwa kwenye Fainali ya 2001.
Katika Mechi 12 zilizopita wakicheza kwao Emirates, Arsenal hawajafungwa hata Bao moja kati Mechi 11.
Liverpool hawajafungwa katika Mechi 9 zilizopita wakishinda 7 na Sare 2.
BRIGHTON & HOVE ALBION v HULL CITY
Brighton na Hull zimekutana mara 2 kwenye FA CUP na Brighton kushinda Mechi zote Mwaka 1985 na 1986.
Katika Mechi 4 zilizopita, wakicheza Nyumbani, Brighton wameshinda zote kwa Bao 1-0.
Hull City, katika Mechi zao 6 zilizopita, wamekuwa wakishinda moja na kufungwa inayofuata na kama hili litaendelea basi watafungwa Mechi hii.
+++++++++++++++++++++++++++++
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
TAREHE ZA RAUNDI:
-RAUNDI YA 3: Jumamosi Januari 4 [KLABU ZA LIGI KUU ENGLAND HUANZA]
-RAUNDI YA 4: Jumamosi Januari 25
-RAUNDI YA 5: Jumamosi Februari 15
-RAUNDI YA 6: Jumamosi Machi 8
-NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
-FAINALI: Jumamosi Mei 17

    



Related Posts:

0 comments: