Sunday, 9 February 2014

MTOTO WA DKT MGIMWA KUPEPERUSHA BENDERA YA CCM UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA



w741 37218
Godfrey Mgimwa, mmoja wa watoto wa Marehemu 
Dkt William Mgimwa, akiongea kwa niaba ya familia wakati wa mazishi kijijini Magunga jimbo la Kalenga mkoani Iringa
Matokeo ya kura za maoni ndani ya CCM yametangazwa 
usiku wa kuamkia leo mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo
 hilo, Godfrey Mgimwa akishinda kwa kishindo katika nafasi 
hiyo huku Jackson Kiswaga akifuatia katika matokeo hayo.
Mtoto wa Mgimwa amepata kushinda kwa kura 342 huku Kiswaga akipata kura 170 na mkuu wa wilya ya Pangani Hafsa Mtasiwa akiambulia kura 42 .
Matokeo hayo yametangazwa katika ukumbi wa shule ya 
sekondari Mwembetogwa Manispaa ya Iringa huku mgombea
 Peter Mtisi akipata kura 33 ,Msafiri Pangagira kura 8,Bryson Kibasa kura 7,Edward Mtakimwa kura 3 na Thomas Mwiluka akiambulia kura 2. Chanzo: Francis Godwin

Related Posts:

0 comments: