Wananchi wa kijiji cha wami Sokoine wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro wamelalamikia kutumia maji machafu yanayotumiwa na mifugoa kwa muda mrefu hali inayotishia afya za wananchi hao kwa kuhofia kupata magonjwa.
Wakizungumza kwa masikitiko wananchi hao wamesema wanalazimika kununua maji shilingi 1,500 kila dumu la lita 20 ambapo wamesema wanashangazwa na hatua ya serikali kushindwa kufanya jitihada za kuwapatia maji wananchi wa kijiji hicho hali ya kuwa wanalipa kodi kama watanzania wa maeneo mengine.
Aidha wananchi hao wamesema kufuatia ukosefu wa maji katika kijiji hicho wamelazimika kutumia nguvu zao kuchimbua Tope lililojaa kwenye bwawa linalotumiwa na mifugo ili kuongeza kina na liwe na uwezo wa kuhifadhi maji kwa muda mrefu ambapo wameiomba serikali na wadau kuwasaidia greda la kuchimbua tope ili kurahisisha kazi hiyo.
Akijibu malalamiko ya wananchi hao kwa njia ya simu diwani mteule wa kata ya wami Sokoine Yusuph Athumani amesema tayari serikali imekwisha anza jitihada za kutandaza mabomba ili kuhakikisha wananchi wa eneo hilo wanaondokana na adha ya ukosefu wa maji.
Chanzo: ITV Televition
0 comments:
Post a Comment