Sunday, 15 November 2015

USHAURI WAKO UNAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YAKE

Nimepokea Ujumbe katika namba yangu kupitia Whatsapp. Huyu binti anaitwa CHRISTINA NOEL anaishi Ilala japo hakupenda nioneshe sura yake, Binti huyu ameolewa na anawatoto watatu (3) wawili wakike na mmoja wa kiume... Binti huyu amekua akipata sana mitihani katika ndoa yake kwa muda mrefu kwa kukosa kuthaminiwa na mume wake na hana furaha na ndoa yake. Na amekua akisikia taarifa za watu wa pembeni wakimwambia kua mume wake anamsaliti katika ndoa yake japo akawa hana uhakika sana kwakua hakua na ushahidi kama mume wake anamsaliti, baada ya taarifa kuenea na kusikia mara kwa mara kwa watu tofauti kua mume wake anamsaliti ikabidi aanze kufanya uchunguzi.

Anasema kua aliwahi kudownload Application iitwayo SOFTBOX TANZANIA katika simu yake, Application ambayo aliipata katika PLAYSTORE na kudownload katika simu yake kwa lengo la kuwa anafuatilia mawasiliano ya mume wake.
Binti huyu alifanikiwa kuingia Playstore na kudownload hiyo Application iitwayo Softbox Tanzania kisha akaunganisha namba ya simu ya mume wake katika hiyo Application na akafanikiwa kua anapata mawasiliano yote ya mume wake SMS anazotuma na anazotumiwa, WHATSAPP CHAT na mawasiliano ya simu anazopiga na kupigiwa binti huyu akawa anapata mawasiliano hayo kupitia hiyo Application pasipo mume wake kujua kama mke wake anapata mawasiliano yake yote.
Katika kufuatilia hayo mawasiliano akabaini kua nikweli mume wake anamsaliti katika ndoa yao kwakua alikua akipokea mawasiliano ya wanawake ambao mume wake alikua anamuhisiano nao!!
Kuna siku binti akapokea mawasiliano yakumshtua ambayo mume wake alikua akiwasiliana na Dokta mmoja wa Hospital ya Mwananyamala ambae Dokta huyu ni rafiki wa Mume wake. Katika Chating zao Dokta na mume wa binti huyu ilionekana kua Mume wa Binti huyu alikwenda Hospital ya Mwananyamala kufanya vipimo vya Ukimwi na kukutwa ameathirika hivyo Dokta alikua kama anampa matumaini na faraja kwa kumshauri katika meseji wakichat pasipo wao kujua kama binti huyu anapata mawasiliano yao.
Binti baada ya kuona vile akakosa amani nakujua tayari familia imeteketea kesho yake asubuh binti huyu akaenda Hospital kupima ili ajue afya yake kama amesalimika, kwa bahati nzuri majibu ya binti huyu yalikuja mazuri nakuambiwa yuko salama hajaathirika.
‪#‎USHAURI‬: Binti haelewi achukue hatua gani kwa mume wake na kutokana na hali iliyojitokeza mumewe ni muathirika ila yeye yupo salama anaomba Ushauri. 
Tusaidie kumpa ushauri
  

0 comments: