Mwanasoka wa zamani wa timu ya taifa ya Rwanda na klabu ya Rayon Sports yaRwanda Hamad Ndikumana amerudi tena katika headlines za soka November 20,Ndikumana ambaye ni mume wa muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya ametemwa na klabu yake ya Stand United baada ya kocha wa timu hiyo mfaransa Patrick Liewigkutohitaji huduma yake.
Ndikumana ambaye alikuwa na klabu ya Stand United ya Shinyanga kwa kipindi cha miezi minne ametemwa rasmi na klabu hiyo, hivyo kwa sasa ni mchezaji huru, awaliNdikumana aliwahi kugoma kuichezea klabu hiyo baada ya kutomaliziwa malipo yake lakini msemaji wa Stand United ya Shinyanga Deokaji Makomba amethibitisha kuwa moja kati ya sababu zilizofanya wamuache staa huyo ni umri wake kuwa mkubwa.
“Kocha amesema hatomuhitaji tena katika kikosi chake sababu kubwa ilitajwa na mwalimu ya kumuacha Hamad Ndikumana ni kuwa na umri mkubwa hivyo mwalimu kaona aachane nae kwani itakuwa ngumu kuendelea nae, Hamad Ndikumana hatupo nae tena na tayari ameshakamilishiwa haki zake” >>> Deokaji Makomba
Ndikumana ambaye amewahi kutamba na vilabu kadhaa anatajwa kuwa na umri wa miaka 37, umri ambao ni mkubwa kisoka, kama utakuwa unakumbuka vizuri Ndikumanandio jamaa ambaye alimuoa mrembo kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo Irene Uwoyana kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume anaitwa Krish.
0 comments:
Post a Comment