Nyota ya beki wa pembeni wa klabu ya Simba SC Hassan Ramadhani Kessy inazidi kung’aa ikiwa ni siku kadhaa tu toka aitwe kwa mara ya kwanza katika katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, tayari ametajwa kuhitajika na mahasimu wa jadi waSimba klabu ya Dar Es Salaam Young African.
Jumapili ya November 8 magazeti kadhaa ya bongo yaliandika kuhusu beki huyo kuwa na uwezekano wa asilimia 75 ya kujiunga na klabu ya Yanga licha ya kuwa mkataba wake bado na Simba haujawekwa wazi unaisha lini. Hassan Kessy kwa sasa yupo Johannesuburg Afrika Kusini na anatajwa kujiunga na Yanga mara atakaporejeaDar Es Salaam. Hizo zilikuwa headlines kutoka katika magazeti ila hii ni kauli ya afisa habari wa Simba Haji Manara.
“Mashabiki wa Simba niwaambie kitu kimoja Kessy bado ana mkataba na Simba, Kessy akisharudi kambi ya timu ya taifa kutoka Afrika Kusini tutafanya nae mazungumzo na ataongezewa mkataba kwa sababu kocha wa Simba Dylan Kerr na viongozi bado wana mipango na Kessy, hivyo Kessy ana mkataba na Simba na hatokwenda klabu yoyote” >>>Haji Manara
Hata hivyo kuna dalili za beki huyo kukaribia kusajiliwa na Yanga hususani tukiwa tunaelekea katika kuanza kwa dirisha dogo la usajili zinapata uzito, kwani kauli ya Haji Manara kuwa akirudi Kessy ataongezewa mkataba kitu ambacho kinadhihirisha mkataba wa beki huyo kuwa umebakiza miezi sita hivyo kisheria Yanga wanaruhusiwa kuzungumza na Kessy bila kuwahusisha Simba.
0 comments:
Post a Comment