Matukio ya ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya Kaskazini yamezidi kuongezeka ambapo katika kipindi cha kuanzia mwenzi january mwaka huu jumla ya matukio 670 ya ubakaji yameripotiwa katika vyombo vya kisheria.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa maandalizi ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia katika mikoa ya kanda ya kaskazini Afande Grace Lyimo na kusema kuwa matukio hayo yanaonekana kuongezeka kutokana na jamii kuwa na muamko wa kutoa taarifa hizo kwenye vyombo vya kisheria.
Amesema katika mkoa wa Kilimanjaro jumla ya matuko ya makosa ya ubakaji yaliripotiwa katika kipindi cha januari hadi oktoba mwaka huu ni 164,mkoa wa arusha ni 164,mkoa wa tanga ni 243 na mkoa wa Manyarani 99 hali ambayo ni tishio licha ya elimu ambayo imeendelea kutolewa katika jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kanda ya Kaskazini meneja Progaramu wa shirika lisilo la kiserikali la kupambana na ukeketaji mkoawa Kilimanjaro (NAFGEM) Honorata Nasuwa amesema mila potofu,imani za kishirikina, ulevi,umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa matukio ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
Nao baadhi ya wanaharakati wa haki za binadamu mkoa wa Kilimanjaro wamesema hatua ya serika kutunga sheria ya matumzii ya mitandao ya kijamii imepunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya uzalilishwaji wa utu wa binadamu ikiwemo watoto na wanawake.
0 comments:
Post a Comment