Monday, 16 November 2015

UKAWA wamtangaza Ole Medeye kuwa Mgombea Uspika

 


Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umemteua, Goodluck Ole Medeye (Chadema) kusimama katika nafasi ya uspika,huku katika nafasi ya unaibu Spika akiteuliwa,Magdalena Sakaya wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mwakilishi aliyekuwa anatazamiwa kuwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kinyang’anyiro cha nafasi ya uspika Mpekuziilibaini kuwa jina la Goodluck Ole Medeye, ndilo lililokuwa likitajwa kuwa litasimamishwa katika nafasi hiyo.

Ole Medeye, aliwahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi kupitia CCM,aliwahi pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete (CCM).

Umoja wa Vyama unaofahamika kama Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

0 comments: