Thursday, 19 November 2015

WAtanzania Rais Kikwete Alishindwa Haya, JE John P. Magufuli Ataweza?

 
Rais Magufuli na Jakaya Kikwete
Maisha bora kwa kila mtu ni sera ya CCM, ambayo kiukweli ni nzuri sana na inaleta matumaini kama ikitekelezwa, ila utelezaji wa sera hii unapambana na vikwazo vingi ambavyo sijui rais John Pombe Magufuli ataviweza, maana mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete vilimshinda kabisa, vikwazo vikuu vya utekelezaji wa sera hii ya maisha bora kwa kila mtu baadhi ni vifuatavyo:-

1.Watumishi wa serikali, hasa wa halmashauri siyo waaminifu (yaani ni one hundred percent corrupt), kwa sababu kutekeleza sera hii serikali kuu inatuma hela nyingi sana kwenye halimashauri za wilaya ambako watu ndiko walipo ili kutekeleleza miradi mbali ya maendeleo. Kule pesa inakutana na watumishi ambao ni corrupt, wanashambulia hela zote za miradi kwa kujenga mabangaloo, wananunua posh cars kwa hiyo miradi ya maendeleo inakwama automatically na sera ya maisha bora kwa kila mtu nayoinakwama.


2.Watumishi niliowataja hapo juu kwa mujibu wa utaratibu wanasimamiwa na madiwani waliopo katika halimashauri hizo, sasa madiwani hao uwezo wa kuwasimamia vizuri hawana kwa sababu elimu zao wengine ni duni sana, hasa madiwani wa viti maalumu. Katika halmashauri nyingi madiwani hawa ni mizigo tu, kwa hiyo watumishi ambao sio waaminifu wanautumia vizuri mwanya huu kuikwamisha sera ya maisha bora kwa kila mtu, kwa kuwalambisha hela kidogo madiwani hawa halafu wenyewe wanakwapua nyingi.


3.Serikali yenyewe kwa ujumla ni dhaifu, inashindwa kabisa kuwachukulia hatua wabadhirifu hawa inaishia tu kuwahamisha toka halmashauri moja kwenda ingine.


4.Idara ya usalama wa taifa(TISS) nayo imezorota sana, kule wanawaona kabisa watumishi ambao siyo waaminifu wanavyofanya wananunua magari mawili mawili na kujenga nyumba kali ndani ya mwaka mmoja tu wa kuajiriwa lakini hawapeleki habari kunakohusika, wanashughulika na mambo yasiyokuwa na tija kama kufuatilia mikutano ya CHADEMA.

Mh. John Pombe Magufuli akiweza kuyadhibiti hayo hapo juu, basi maisha bora kwa kila mtu inawezekana.

By laurent Msembeyu/JF

0 comments: